Ushauri: Kuoa mwanamke aliyezaa na wanaume wawili tofauti na mimi niwe wa tatu

krava

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
225
287
Kuna faida na hasara gani kuoa mwanamke aliyezaa na wanaume wawili tofauti mimi nikimuoa nitakuwa mwanaume wa tatu na nikizaa nae atakuwa amezaa watoto wa Tatu kwa baba watatu.

Je hii inakuwaje?

Ni kawaida au, msaada please
 
Wewe ndio unaejua mazingira halisi na hali iliyopo. Kuja kuomba humu ushauri ni kutafuta sababu tu za kumuacha.

Jiulize moyoni je wampenda? Kama unataka ushauri wa kweli omba kwa wazazi wako au ndugu zako wa karibu unaowaamini.
 
Wewe kama umempenda na umeona ndio anayekufaa muoe tu mkuu haya mambo hayana formula maalum.Unaweza ukaoa ambaye hana hata mtoto mmoja akaja kuzaa akiwa ndani ya ndoa na wanaume wengine ukabakia unaitwa baba jina.Muombe Mungu wako akuongoze katika hilo.
 
Kwanza wewe ni mtu wa maana sana. Unajua wazi kabisa umeenda kuchukua "Used" ukaona uchukue used kabisaaa bila chenga. Pili uliwaona watoto wake watakaokuwa wako baadae. Sasa swali lako la nini na kwa nani?? Kwani tutakuwa na weye chumbani??
 
Dah tatizo hakuna si umependa..
Ila kumbu kuna siku atahitaji awe faragha na wazazi wenzie..
Akili kumkichwa mkuu usijaribu imani zetu
 
Sikiliza moyo wako Muombe Mungu hakuna mkamilifu oa Lea watoto hutaishi milele hapa dunian hakuna ambae hagongewi labda kama na wew hugongi ndoa ni kuvumilia situesheni sio kuzuia hvyo songa kaka
 
Mbona Diamond 'kaoa' mwanamke aliyezalishwa watoto watatu na bado anakula bata? Mkijipanga tu mkaelewana vizuri, maisha yanasonga...
 
Ni mtihan huo mkuu ila acha moyo wako uamue apa utapata stress tu wengi umu wamevurugwa na tarehe ya Sayansi na Hisabat lini
 
We ndio unamfahamu huyo mwanamke na kilichokusukuma kumpenda hata kumtongoza na kutakaawe mkeo, kwahiyo kama huwezi kutafakari na kutafuta peoples openions kuendesha maisha yako basi kazi ipo.
 
Kama umempenda na unania ya dhati ya kumuoa basi usiogope,ujana unamambo mengi.

Huenda ni mwanamke mzuri ila wanaume aliokuwanao hawakuwa na msimamo thabiti.

Just set your rules make her Happy.
 
Wewe kama umempenda na umeona ndio anayekufaa muoe tu mkuu haya mambo hayana formula maalum.Unaweza ukaoa ambaye hana hata mtoto mmoja akaja kuzaa akiwa ndani ya ndoa na wanaume wengine ukabakia unaitwa baba jina.Muombe Mungu wako akuongoze katika hilo.
Hahaha mkuu umezunguza kiume kwa herufi Dume na maandishi ya jinsia ya kiumeniii
 
Kufahamu ni jambo moja ndugu, waweza kukutana na mwingine na ukaoa na wala usijue kama aliwahi kuzaa na akamtelekeza Mtoto, au la alim/watupa chooni, leo akisimama mbele yako msaaaafi.

As long as binaadamu tuna kikomo cha upeo mengine tumuachie Mungu...kama mnaelewana na mwenzi wako muoane tu muendeleze familia.
 
Kuna faida na hasara gani kuoa mwanamke aliyezaa na wanaume wawili tofauti Mimi nikimuoa nitakuwa mwanaume wa tatu na nikizaa nae atakuwa amezaa watoto wa Tatu kwa baba watatu je hii inakuwaje? Nikawaida au msaada plz
Angalia movie Inaitwa Daddy's Home. Utapata maamuzi mazuri baada ya kuangalia.
 
Back
Top Bottom