uzeebusara
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 657
- 514
Habari zenu wana Taaluma humu ndani
Nina jambo naomba nanyi mnipe ushauri wa kumsaidia mdogo wangu.
Nina mdogo wangu wa kiume ambaye kamaliza kidato cha sita katika haya matokeo yaliyotoka hivi karibuni mwaka 2016. Huyu kijana alichukua mchepuo wa EGM na matokeo kwa kweli sio mazuri kwani amepata S, D na E. Tuliyapokea nyumbani na wazazi na kumshukuru Mwenyezi Mungu ingawaje ukweli hatukutarajia sana afeli hivyo japo hawa vijana wa sasa wa kushinda katika social media lolote yakubidi ulipokee.
Sasa, mimi kama kaka mkubwa nikaambiwa tufanye nini kumsaidia kumwendeleza kwani kwa mujibu wa ule waraka wa NACTE kijana huyu hana sifa za kujiunga chuo kikuu moja kwa moja. Nikatoa ushauri aanzie ngazi ambayo itaendana na alama alizopata. Ngazi hiyo yaweza kuwa labda stashahada au stashahada ya juu ilimradi tu tumuhangaikie kumuendeleza asikae nyumbani. Wazo la kukariri mtihani kwa kweli mimi sikuliafiki japo mzazi wangu alilitoa kwani kwa mtazamo wangu na uzoefu nilionao mwanafunzi kama alishindwa kufauli wakati yupo shuleni mazingira ya kielimu yanamshughulisha na taaluma siamini akikaa mtaani ataweza. Na huyu kijana alikiri hatoweza kwa hili la kukariri masomo.
Sasa yeye kaja na suala kwamba anaamini ameonewa katika kusahihishiwa mitihani yake hasa somo la Jiografia. Kwa mimi hii haiingii akilini kabisaaa na sikubaliani na hili zaidi ya kuona anataka kuongeza gharama bila sababu. Kigezo nachotumia hapo ni masomo mengine vilevile naona kabisa hajafanya vizuri sasa hili la rufaa si hasara jamani. Anyway naombeni ushauri labda nimweleze au nimpe ushauri gani ataelewa ili tusonge mbele maaana kang'ang'ania sana na kikao ni leo jioni. Pili, kwa ambao wanafahamu au uzoefu wa masuala ya kukata rufaa naomba kujua taratibu na gharama zipo vipi! Vile vile pannel ya wanaosahihisha upya wapo strict kiasi gani!
Nawasilisha