Ushauri kuhusu kugombea ubunge 2015.

boby v

Member
Jul 25, 2012
30
0
Habari yenu wana jf. Mimi ni kijana wa miaka 25 nina ndoto ya kugombea ubunge huko mahenge katika jimbo linaloongozwa na mh. Selina kombani wa ccm. Mimi ni mwanachama wa chadema, ila sina elimu ya juu elimu yangu ni ya msingi. Nifanyaje sasa wana jamii? Naomben ushauri wenu.
 
Sifa ya kuwa mbunge ni ujuwe kusoma na kuandika tu. Elimu ya Msingi kwa Wabunge hawa wanaolala Bungeni ni Elimu kubwa sana.
Maji marefu kaishia darasa la Nne.
Lusinde Elimu ya Msingi.
Deo Sanga Elimu ya msingi.
Jipange tu una sifa zote za kuwa mbunge kama wasi wasi wako ulikuwa ni huo tu.
 
Habari yenu wana jf. Mimi ni kijana wa miaka 25 nina ndoto ya kugombea ubunge huko mahenge katika jimbo linaloongozwa na mh. Selina kombani wa ccm. Mimi ni mwanachama wa chadema, ila sina elimu ya juu elimu yangu ni ya msingi. Nifanyaje sasa wana jamii? Naomben ushauri wenu.

Mkuu upo sawa kabisa. hilo jina Kombani lisikutishe. unachotakiwa ni kuwa mwaminifu, mkweli, jasiri, kuwa na uthubutu na kujitahidi kuyaelewa matatizo ya msingi ya watu wa jimbo lako na nchi kwa ujumla na uumize kichwa kufikiria utawasaidiaje kwa fikra zako na nguvu zako kuwakwamua kwenye matatizo yanayowakabili. Hakikisha una uwezo wa kuwashawishi wananchi wa jimbo lako kuwa wewe utashirikiana nao kwa dhati kutatua kero zao. Tunahitaji sana mchango wako wa dhati kwa taifa letu, elimu yako isikunyongeshe sana, ila uwe tayari kukubaliana na maamuzi ya chama wakati muda utakapowadia, maana chama kinaweza kuamua kusimamisha mgombea mwingine na sio wewe. Uwe tayari kuunga mkono maamuzi hayo na ubaki mwaminifu na mtiifu kwa chama usiwe msaliti.
 
Back
Top Bottom