Chanzo cha maji kilichopo ni tingatinga na kitakacho fanyika ni kuchimba Kisima kandokando ya tingatinga hilo. Maji ni ya uhakika.
.
Kama maji ni ya uhakika basi ni vyema
Ardhi ni tifutifu kuna sehemu nyingine udongo umechanganyikana na changalawe ndogondogo. Shamba lipo kwenye mwinuko.
hapa unauwezekano wa kutumia drip irrigation.\
Kahawa na maharagwe yamelimwa ktk shamba moja. Plot ya shamba la Migomba imelimwa na maharagwe pia. Kuna plot ya maharagwe peke yake. Mikakati ya baadaye; Mahindi kulimwa plot yake pekee, kulima mazao ya vitunguu, nyanya, kabeji, miti ya matunda nk. Hivi vitalimwa ktk plot zinazo jitegemea pekee.
Je hukomvua zikoje?? sijajua una capital kiasi gani kwa ajili umwagiliaji ila kwa hali ya shamba ilivyo na hali halisi ya huko... ushauri wangu ni kama ifwatavyo:
1. Njia za umwagiliaji.
Kwa sababu hakuna umeme, nakushauri utumie drip irrigation ya tank (by gravity), chakufanya uwe na pump yoyote utayotumia kujaza maji kwenye tank lako ambalo litakua juu kwa urefu flani, then kutoka kwenye tank utayapeleka shambani kwa drip system. Katika maelezo yako umesema una uwezo wa kupata pump ya solar au wind, japo zitakua na gharama kubwa kiasi ya kuanzia, ila ukipata moja wapo itakua msaada mkubwa kwako kwa muda mrefu!! incase ukiwa na pump ya solar au wind yenye uwezo mkubwa unaweza unganisha hata spinkler irrigation system (japo sishauri sana uitumie hii katika shamba lenye mwinuko).
Drip itakufaa sana kwenye mazao kama maharage, mahindi, nyanya, kabeji na mazao yote ya muda mfupi. Lakini simaanishi kwamba huwezi tumia drip kwenye kahawa na migomba la hasha...
Tofauti na drip, kwa sababu umesema huko hamna umeme na kuna chanzo cha uhakika cha maji, unaweza pia tumia furrow irrigation (umwagiliaji wa mifereji) hasa kwa mimea kama kahawa na migomba!
Je pump yako ya maji ina uwezo gani?
Usisite kuuliza kama una swali, karibu!