Ushauri kuhusu biashara nzuri ya kufanya, nina mtaji wa laki tatu

Miss Jay

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
211
174
Habari wana jamvi?

Natumaini mu wazima wa afya na Mungu anaendelea kuwalinda.
Nimekuja hapa kuomba ushauri wenu kwa wazoefu wa mambo ya biashara,,ningependa kupata ushauri ni biashara gani naweza kuanzisha kwa mtaji wa milioni 3.

Nisingependa kuchukua mkopo sehemu yoyote hadi pale biashara yangu itakapokuwa kubwa kwaiyo nataka nianze na mtaji ambao ninao mkononi sio wa mkopo.Natumai mtanishauri vizuri na ushauri wenu utanisaidia kufanya maamuzi.
Asanteni.
 
Laki tatu or Million tatu?.Kichwa cha habari kinasema Laki tatu,ndani ya maandishi unasema million tatu?.

Upo mkoa gani?,kijijini au mjini(mkoani au wilayani).
 
kama nimekuelewa vizuri umesa ml.3 ninyingi sana kama upo Mkoani na unapoishi ni kwako wewe usipate taabu ingia kwenye Ufugaji wa kuku wa kienyeji itakutoa ukianza na kuku 200 baada ya miezi sita majibu utayaona
 
Mtaji ni milioni 3 sio laki 3 wapendwa ila nimejaribu ku edit title nimeshindwa
 
Mtaji ni milioni 3 sio laki 3 wapendwa ila nimejaribu ku edit title nimeshindwa
Kandamiza kwa kidole maada yako watakuletea kivuli kwenye mada na sehemu ya juu watakuwekea kama penseli bonyeza pale halafu ndo ndo utaletewa mwendelezo wa kuandika wa ujumbe wako!!!
 
mil tatu ni nyingi kwa kuanzia sehemu uliyopo tafuta chumba maeneo yanayojengeka thn fungua duka dogo la hardware anza na uuzaji wa cement na chokaa na misumali then utaongeza bidhaa kutokana na mahitaji na mzunguko wa biashara. kumbuka biashara hadi iwe stable huwa inachukua miez sita hata mwaka so uwe mvumilivu na nidhamu ya matumizi ya pesa ya biashara
 
Back
Top Bottom