sina imani na haya makitu nyota. ni uzumbukuku na ulimbukeni tu. Ama kweli imani ni jambo la ajabu sana.
Hata sijui nyota zinafanyaje kazi
mmwambie kijana aache kufuata nyota aanze kufuata mwezi akishindwa ajaribu jua
mmwambie kijana aache kufuata nyota aanze kufuata mwezi akishindwa ajaribu jua
mmwambie kijana aache kufuata nyota aanze kufuata mwezi akishindwa ajaribu jua
sipendi kufundisha watu imani za kijinga hapa ila kwakuwa nimevutiwa na uandishi wako umewasilisha mada vizuri, mwambiye mdogo wako abadilishe jina lake ambalo nyota zitakubali na mchumba wake au mchumba abadili jina rasmi kiukweliukweli na asitumie tena jina la zamani na pia aende hadi serikalini kubadilisha jina lake rasmi.
ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ya jambo hilihili kwa sababu wengi hatuamini ukweli wake.
hawa watu wa nyota kwenye biblia wanaitwa mamajusi, wao ndio walikuwa wa kwanza kujuwa kwamba yesu amezaliwa baada ya wao kuiona nyota ya mashariki, hivyo walifunga safari kuifuata nyota hiyo ili kwenda kumsujudia.
mwenye masikio na asikie.
zina kazi kubwa sana, kila siku hapa mmu tunajifanya mabingwa wa kushauri ndoa zenye migogoro kumbe nyingine tatizo kubwa kuna hizi nyota kamwe haziwezi kukaa pamoja.
hivi hamjawahi kujiuliza ni kwa nini hata kampuni pia huwa zinabadiri majina? hapa siongolei yale majizi yanayokwepa kodi.
Ni kweli mwambie abadili jina mume au mke ila kwa sababu mume ni kichwa cha familia mwanamke ndio anatakiwa kubadili ila asimwambie mambo mengi yakamchanganya mke, kama anabisha ushauri wa kwanza mwache aoe lakini wanaweza wasidumu au wasichume maisha yao yakawa ya tabu. Hata TB joshua alitabili ndege itaanguka wawe makini, na ikaanguka na mengine mengi kama ya wasanii mwaka huu wanavyowahi viwanja.
Mkuu mi ni mshamba sana wa elimu nyota. Kwa kaujuzi kangu kadogo nilikuwa najua nyota zihusishwa na tarehe za kuzaliwa. Sasa kubadili jina tena inafanyaje nyota ya mtu kubadilika?
Ata badili jina lakini nyota yake itabaki kuwa palepale sababu tarehe ya kuzaliwa hakuna anaeweza kuibadili atabadili kwenye cheti bt ukweli utabaki kuwa pale pale
Mkuu Matola, nadhani ingekuwa ni bora ukatiririka humu namna hizo nyota zinavyofanya kazi. Uelezee kuoana na kuto kuoana kwa hizo nyota ili tuelewe specifically nini kinamaanishwa hapa.:israel:
mkuu wewe ni mmoja ya watu makini jukwaa hili, nimesoma vyema mleta mada yuko serious ni vizuri kama tutamsaidia.
cc: MziziMkavu