Ushauri kiafya

kiganana

Member
Jun 26, 2016
12
7
Habari wanajamvi!
Naomba ushauri,nimejiuliza muda mrefu sana na Leo nimeamua kupiga moyo konde kuuliza ili kupata ushauri utakao nipa ahueni ya maisha...
Umri wangu unaanzia na namba3, utata huu ulianzia mwaka 2009 nikiwa mwaka wa kwanza chuo kikuu kimoja hapa nchini,nlikutana na binti tukaanzisha uhusiano...akapata ujauzito...tulikwenda wote clinic na tukapimwa afya tukakutwa wazima...mwaka 2011 December 1 siku ya ukimwi nlienda kupima pale chuoni .. Nikaambiwa nikae nje kusubiri..nkasubiri na kuitwa baada ya dakika chache...wakanihoji kama natumia sana kilevi nkawambia ndio wakaomba nipime tena nkakubali....lakini sikurudi tena mara ya pili kupewa majibu...tukamaliza chuo nami nkaenda mkoa mmoja kutafuta life huko mambo yalikua mengi huo ni mwaka 2012...kuna usiku mmoja nikachukua kakipimo ka kujipima ukimwi na kakatoa vimistari 2 kiashiria kua kimedetect...nlixhanganyikiwa ila nkajipa moyo kua labda in sababu ya ulevi kama nlivyoambiwa awali.
Tangu hapo nimeendelea na maisha na mahusiano na yule mama mtoto wangu lakini tukiwa mbali...nimekua nakuja naye aja nlipo....mwaka Jana mwezi may nkakutana na binti mwingine tukaanzisha mahusiano.....akapata ujauzito na tukaenda clinic kupimwa mie nkaonekana nimeathirika ila yeye mzima....tukakuza na sasa tunamtoto mwenye afya njema...nimekua naendelea na maisha bila ya kupata dalili zozote za ugonjwa...nimekua nasumbuliwa na malaria na so Mara kwa Mara. Je huchukua muda gani MTU kuanza kuteseka?nisaidieni mini nifanye?nimekua na mahusiano na wasichana kadhaa na hakuna aliyeumia wengi wameolewa na wana watoto....

Karibuni
 
Muone daktari, ufanyiwe vipimo ili kama kuanza dawa uanze...., kuna faida lukuki za kuanza dawa kwa muda muafaka. By the way, jipe moyo...., ni gonjwa kama yalivyo magonjwa mengine. Kuna magonjwa yenye mateso zaidi ya ukimwi..., ni mtihani though, ila jaribu kuwa positive minded. Above all, walinde wengine...., hiyo habari kuwa wapo sawa haivutii kuisikia.

Thanks
 
Back
Top Bottom