Ushauri: Kaweka Picha ya Mwanamke Mwingine kwenye Profile yake lakini bado ananitaka

Sabry001

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,064
354
kuna mtu anahitaji msaada wangu na nahisi siwezi kumshauri vizuri sana kutokana na itikadi zangu dhidi ya wanaume.

Huyu dada kanijia, alikuwa na mpenzi wake wamekaa wote kwa miaka 2 na walikuwa vizuri tu, mwaka huu May uliibuka mjadala kati yake na huyu kijana kwamba anataka amzalia mtoto mmoja, yule dada akanijia nami nikamshauri kuwa asikubali kubeba mimba kabla hajafunga ndoa kwani malezi ya mtoto bila kuwa na baba yake karibu sometimes yanakuwaga mazito.

alimweleza baby wake kuwa mpaka wafunge ndoa ndipo atakapobeba mimba, the guy is now 38 na alimwambia binti kuwa hana haraka ya kufunga ndoa as ana mambo anaweka sawa. nilimshauri vya kumashauri na mahusiano yakaenda kama kawaida.

agosti mwaka huu binti alipata safari ya kikazi na alimuaga mpenzi wake vizuri, baada ya wiki moja binti aliona mwanaume wake amemweka manzi mwingine profile pic wasap, alipomuuliza uliibuka mgogoro mkubwa sana ambao ulipelekea kurushiana maneno makali baina yao na sms zote niliziona aliporudi alinionesha.

BInafsi nilikasirika ila huyu binti anaonekana anampemda sana mwanaume wake. PIcha ilikaa tangu agost mpaka mwishoni mwa september yule kaka aliweka picha nyingine amekaa na huyo manzi mpya somewhere wanakula bata. Huyu rafiki yanghu alilia sana na nilijaribu kumshauri ila simanzi ya moyo mwaijua wenyewe.

Muda ulipita na yule kijana aliomba kuonana na yule binti, walionana na yule kaka alikiri kuwa bado anampenda yule dada but anahisi amelogwa na huyu manzi mpya hivyo anamuomba huyo dada amuombee kwa Mungu ili afanye maamuzi sahihi. walikaa wakaongea na baadae wakatawanyika kila mtu kwao.

YUle rafiki yangu alikuja kwangu analia maana alikuta jamaa kaweka picha ya manzi walpaper na walipiga simu akiwa hapo na jamma aliitika Hallow my Happiness(yaani manzi mpya ndio happiness yake)

Nilimshauri na November yote alikuwa anauguza jeraha na alikuwa ameamua kusonga mbele ila this week jamaa amempigia binti simu anataka aonane nae kuna mambo hayendi vizuri.

Nilikaa na huyu dada nikamsaidia kureply some sms toka kwa kijana na inavyoonesha kule ni aliingia choo cha kike hivyo anataka kurudi kwa gear ya kutaka ushauri kwa binti. mie nimemwambia kwa uzoefu wangu na mijanaume hasa isiyo na staha, anataka asingizie kuwa huko ni kugumu ili awakule wote kwa pamoja. huyu rafiki yangu kwa vile anampenda sana jamaa yake anasema anataka kwenda kuonana nae kwa maana anampenda sana, hofu yangu asije akaumia tena au akachanganywa na mwishowe akabwagwa tena.

Sasa basi kwa kuwa mie sinaga ushauri mzuri sana hasa unaohusu wanaume waliojichetua kama huyu zaidi ya kusema achana nae, naombeni mutoe ushauri wenu nami nitamuonesha kama ulivyo... nae achanganye zake na za kuambiwa afanye mambo.

Asanteni
 
Last edited by a moderator:
Huyu jamaa ana miaka 38 bado kuna mambo anapanga. Akifikisha 40 ataendelea kupanga tu. Huyu jamaa wala hana mpango wa kuoa bali apate mtoto na amlee mtoto basi aendelee na kula maisha na akishapata mtoto ndio mwisho wa habari ya kuona tena. Lakini kun awengine ukimzalia mtoto kama anakupenda bado huyo mtoto anaweza kuwaunganisha haraka kuliko ilivyo sasa. Yeye ndio anamuelewa zaidi huyo jamaa.
 
Huyu jamaa ana miaka 38 bado kuna mambo anapanga. Akifikisha 40 ataendelea kupanga tu. Huyu jamaa wala hana mpango wa kuoa bali apate mtoto na amlee mtoto basi aendelee na kula maisha na akishapata mtoto ndio mwisho wa habari ya kuona tena. Lakini kun awengine ukimzalia mtoto kama anakupenda bado huyo mtoto anaweza kuwaunganisha haraka kuliko ilivyo sasa. Yeye ndio anamuelewa zaidi huyo jamaa.
Asikatae wito. Akatae asilolitaka
 
Huyo besti yako wala hana haja ya kushauriwa chochote. Wa kushauriwa ni wewe mleta mada, kuwa unatakiwa kukaa mbali na uhusiano wa hao watu. Akija we msikilize kama mtu wako wa karibu baas
 
Mwambie aache ujinga, yeye sio wa kwanza kupenda hapa duniani. .. huyo bwana anaweza kumzalisha na kumpotezea na inawezekana mpk sasa ana mababy mama kadhaa wapo watu wa hivyo wasiotaka majukumu lkn wanataka watoto.
Pili, huyu "man friend" umri wake sio wa boyfriend hapo hawezi kusema hajajipanga labda kwamba hajajipanga kumuoa huyo shoga ako.
Tatu, anafanya hivyo vitu awe na chances kote kote, anajifanya amelogwa huo ni uongo wa wanaume chupi mkononi wakifumaniwa na wanawake. Huyo wa kwenye profile pic na wallpaper ameahidiwa vingi zaidi ya shoga ako.
Mwambie a move on, a dog is just a dog even when u call it bobby brown.
Mtu anayekupenda hawezi kukufanyia hivyo, asijidhalilishe kuendelea kujikombekeza zaidi.
 
Huyu jamaa ana miaka 38 bado kuna mambo anapanga. Akifikisha 40 ataendelea kupanga tu. Huyu jamaa wala hana mpango wa kuoa bali apate mtoto na amlee mtoto basi aendelee na kula maisha na akishapata mtoto ndio mwisho wa habari ya kuona tena. Lakini kun awengine ukimzalia mtoto kama anakupenda bado huyo mtoto anaweza kuwaunganisha haraka kuliko ilivyo sasa. Yeye ndio anamuelewa zaidi huyo jamaa.
Mie ndo nashangaaa kikongwe kama huyu bado anang'aa sharubu mpaka leo.
 
Hua napata tabu sana kuwaelewa wanaume wa aina hii, 38 years na bado ana ruka ruka tu kama mtoto wa mbuzi, badala ya kuwaza kufunga ndoa na kujenga family yeye ndo kwanza ana donoa huku na huko na kuforce kupata mtoto nje ya ndoa, hivi hua ni ugonjwa au ni nini?na hapo unakuta kapata binti anayestahili kua mke but bado wala hana habari, katika hali ya kawaida mwanaume wa 38 yrs anapaswa kua na mke na watoto. Mwambie rafiki yako kama hawezi kufanya maumuzi sasa ipo siku atajuta and itakua too late.
 
Huyo dada naye anagonga hodi kwenye miaka 40 nini?

Yaani mtu upo naye anakosa uaminifu waziwazi bado unamganda.
 
Hivi kuna watu akili zao ziko wapi. Mwambie huyo rafiki yako asiwe mjinga. Mjini hapa
 
Back
Top Bottom