Ushauri kati ya M.A kiswahili na M.A linguistics

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
3,643
Reaction score
4,182
Wakuu,

Pamoja na kuuona ugumu katika kutafuta nafasi ya Tutorial Assistant upande wa Kiswahili/Kiingereza,

Bado nina nia na malengo ya dhati ya kuwa mwanataaluma mbobezi wa ama Kiswahili au Kiingereza(Linguistics).
______
Matakwa yangu ya awali ni kufanya
M.A(Linguistics)
Kwani naiona ni kozi ambayo haina ushindani mkubwa kutokana na ukweli kuwa watu wengi hawapendi kuisomea kwa kuhofia ugumu wa hiyo kozi,
Hivyo uwezekano wa kupata fursa kama Assistant Lecturer waweza kuwa mkubwa.
Ila changamoto kubwa ni ada yake ipo juu (kwa uwezo wangu kiuchumi).

Mbadala wake,
Nafikiria kusomea M.A(Kiswahili) kwani ada yake ni affordable kidogo ikilinganishwa na ya M.A(Linguistics).

Ila wasiwasi wangu ni kwamba,
Hii M.A(Kiswahili) yaweza kuwa na watu wengi sana halafu ikaleta changamoto kubwa kwenye kupata nafasi ya Assistant Lecturer kwa upande wa Kiswahili.

OMBI:
1. Kwa anayejua asasi zinazotoa ufadhili wa kozi za Umahiri naomba anipe dondoo,
Ili nijaribu kuomba ufadhili kwa ajili ya M.A(Linguistics).

2. Mliopo kwenye hizi kada,
Uhalisia upoje hasa kwenye kupata nafasi (za kazi) za fani hizo huko vyuoni hasa kwa upande wa Kiswahili ambako naweza kuzichanga nikaanza masomo kwa mwakani.

3. Upi ni uhalisia kulingana na hizo fikra zangu?

Tanbihi:
KIUKWELI,
LENGO LANGU KUU LA KWENDA KUSOMEA MASTER NI KUTAFUTA NAFASI YA KUWA MHADHIRI WA ELIMU YA JUU.

NATARAJIA KUOMBA UDSM/UDOM MWAKANI TUKIJAALIWA.

Karibuni kwa ushauri, changamoto na mawazo wakuu.
 
lakini katika first degree yako huna GPA ya 3.8 and above maana bila hivyo uwezi kuwa mhadhiri katika vyuo hivyo
 
Nakushauri fanya M.A ya kiswahili coz wasomi wengi wa hii coz hapa nchini wanatoka kenya kwa mfano walimu wengi wa kiswahil saut ni wakenya so ukimaliza unaweza kuwa mmoja wa watanzania pekee kupata kaz saut
 
AHSANTE MKUU,
NIMEUCHUKUA USHAURI WAKO.

NGOJA TUPATE NA MAWAZO YA WENGINE!
 
Mie kwa mtazamo wangu M.A (kiswahili) ni muafaka zaidi kwani nadhani umeona juhudi za serikali na taasisi za elimu ya juu kukihuisha kiswahili mfano chuo kikuu cha Dar es salaam wametangaza kutumika kwa kiswahili kwa mawasiliano ya pale ndani hivyo kutahitajika wamilisi wengi na wabobezi wengi katika uwanja wa taaluma hii ili kufikia malengo hayo.
 
NIMEKUELEWA VEMA MKUU.

AHSANTE SANA KWA MCHANGO WA MAWAZO.
 
Back
Top Bottom