Habari zenu wakuu,
Mimi ni kijana wa kiume niliyezaliwa katika familiya ya watoto watano, nimeajiriwa serikalini nina kaka yangu yeye hakusoma yuko yumbani anaishi na wazazi, huyu kaka yangu ni mtu wa makamo ana umri wa miaka thelathini na ushee kwa kweli amekuwa akiendekeza kunywa pombe muda wote akinywa pombe yaani ni vurugu na fujo yaani nyumbani hakukaliki.
Tumejaribu kumsihi na wazazi kumkanya lakini wapi, siku karibu zinazokwenda amekuwa mgomvi na mnywaji pombe wa kupindukia na mwenye matusi hata mama mzazi wakuu nimfanyaje ili abadilike nimejaribu kumsaidia kumpa pesa afanye biashara lakini ameishia kuinywea pombe na hakikosa pesa huwa anaiba mpaka ndani au kuuza vitu ili akanywe pombe. Ndugu wengine wameshamchoka na alishafanyiwa maombi lakini wapi na walishampeleka kwenye kambi moja ya malezi ya kidini alibadilika lakini baada ya muda kabadilika.