Ushauri Juu ya Kununua UPS.

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,280
Wadau wa jukwaa hili:Habari zenu?
Mimi ninaishi sehemu ambayo umeme unakatikakatika ovyo sana. Kila ukikatika unarudi baada ya dakika ishirini au nusu saa. Tatizo hili linanikera sana maana kilaptop changu kina betri moja na umeme ukizima meseji inatokea kunieleza kwamba betri imeisha haina nguvu. Dakika tano tu baada ya umeme kukatika laptop inazima.

Sasa wataalamu wangu, kwa mawazo yangu,nimeonelea ninunue UPS ili niepukane na adha hiyo.Je wazo langu ni sahihi na je ni zipi specifications muhimu za ups inayonifaa?

Ni hayo tu wataalamu wangu naomba msaada wa ushauri.

Laptop yangu ni HP 530 Notebook
 

me ninayo UPS lakini kwanini usitafute betri mpya ya laptop yako badala ya UPS?
 
bwana HYGEIA ups haiongezi muda wa kukaa na chaji, ups inakupa nafasi kuzima vifaa vyako kikawaida pale umeme unapokatika, kwa hiyo hata ukinunua ups bado laptop yako haitakaa na chaji, labda ununue battery mpya ili ikae na chaji kwa muda mrefu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mie nakushauri nunua battery ya laptop hiyo kwa kiasi kiasi kisichozidi TZS 80,000/=
Kama una UPS au utapata kwa bei chee chukua APC 750 ambayo inauwezo wa kukuweka kwenye Power kwa Dakika sizizopungua 45 kwa vitu vifuatavyo vikiwa on Laptop,TV(LCD 27") na Decoda 1 + charger za simu 3
 
Mkuu tafuta APC legendary Reliability (230V Model 750). Hiyo Smart - UPS ni kitu cha Philippines kimetulia hata zaidi ya saa unaendelea kutesa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tafuta APC legendary Reliability (230V Model 750). Hiyo Smart - UPS ni kitu cha Philippines kimetulia hata zaidi ya saa unaendelea kutesa.
Asante grafani 11. Je, zinapatikana hapa bongo?
 
Last edited by a moderator:
bwana HYGEIA ups haiongezi muda wa kukaa na chaji, ups inakupa nafasi kuzima vifaa vyako kikawaida pale umeme unapokatika, kwa hiyo hata ukinunua ups bado laptop yako haitakaa na chaji, labda ununue battery mpya ili ikae na chaji kwa muda mrefu
Halo @C6. Mbona unanikoroga? Yaani wataka kuniambia kwamba ups haitaniruhusu kuendelea kufanya kazi na kompyuta yangu pale umeme unapokata?
 
Halo @C6. Mbona unanikoroga? Yaani wataka kuniambia kwamba ups haitaniruhusu kuendelea kufanya kazi na kompyuta yangu pale umeme unapokata?

naunga mkono hoja ya C6 UPS ni kwa ajili ya destop na power backup yake ni dk 5 na bei ni elfu70 sasa si bora ununue betri ya laptop tu.
 
Halo @C6. Mbona unanikoroga? Yaani wataka kuniambia kwamba ups haitaniruhusu kuendelea kufanya kazi na kompyuta yangu pale umeme unapokata?

itasaidia vifaa visizimike ghafla umeme unapokatika, wala ups haiweki umeme muda mrefu "uninterupted power supply"
 
Nafikiri hii hoja inamikwazano na wadau ambao waliofundishwa na kushika ya kuwa UPS ni kwa ajili ya Desktop tuu? poleni sana wadungu na mnahitaji kuongeza kidogo Elimu kuhusu UPS.

Unajua unaweza kuwasha taa zako kadhaa za energy server na UPS bila kuichakachua UPS?

APC 750VA mpya pale mlimani city duka opp na NMB bank wanauza TZS450,000(6 ports power backup)
APC 650VA mpya wanauza kwa TZS 180,000(3 ports power backup)

Za kichina kuanzia elfu 70,000 unapata ups ya 650VA

ila mtaani kwa Elfu 80 hadi 100,000 unapata kulingana na ubora wa battery.
 
Naomba kuunga hapa wakuu! Kuna UPS ambazo zina kuza volts za umeme mfano: nina sola inayozalisha volts 12 naweza unga ktk UPS nkapata 220v au watts?
 
bwana HYGEIA ups haiongezi muda wa kukaa na chaji, ups inakupa nafasi kuzima vifaa vyako kikawaida pale umeme unapokatika, kwa hiyo hata ukinunua ups bado laptop yako haitakaa na chaji, labda ununue battery mpya ili ikae na chaji kwa muda mrefu

naunga mkono hoja ya C6 UPS ni kwa ajili ya destop na power backup yake ni dk 5 na bei ni elfu70 sasa si bora ununue betri ya laptop tu.
Hivi nyinyi waheshimiwa mnaelewa vizuri UPS na kazi zake au mnafikiri ni sawa na taa za kuchaji.

Mnaifahamu APC legendary Reliability (230V Model 750) vizuri kweli? msilinganishe Yutong zenu za shilingi elfu kumi na tano na mashine hiyo. Kama una laptop tu hata umeme ukatike unaweza piga mzigo kuanzia dakika 40 na zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Hapo utakuwa unaongelea kitu kingine kabisa, tafuta wataalamu wa Inverters.
Naomba kuunga hapa wakuu! Kuna UPS ambazo zina kuza volts za umeme mfano: nina sola inayozalisha volts 12 naweza unga ktk UPS nkapata 220v au watts?
 

mkuu me nimeshauri mtoa mada atafute battery ya laptop kupata UPS itayokaa na chaji saa 1 au zaidi (kama ipo) itam-cost sana.
 

wewe hujui unachokisema afu unapanic, habari iko hivi,

1. kumshauri mtu mwenye laptop anunue ups badala ya battery uo ni uchizi....

2. ups kuweka umeme dakika 40 sio ishu, unajua kazi ya ups? soma hapa chini...

A UPS is typically used to protect hardware
such as computers, data centers,
telecommunication equipment or other
electrical equipment where an unexpected
power disruption could cause injuries,
fatalities, serious business disruption or
data loss.

source: http://en.m.wikipedia.org/wiki/Uninterruptible_power_supply
 
Hizo kazi ulizakariri leo tulizifahamu miaka mingi kabla ya wewe kujua kutumia mtandao na kufungua hiyo source yako.

Halafu nafikiri hujaelewa maana halisi ya uchizi. Kipi ni uchizi, kumshauri mtu kitu alichouliza ili apate taarifa zake sahihi au kumtoa nje ya mada na kumlazimisha kununua kitu kingine kama ulivyofanya wewe? kwani mtoa mada alikwambia anataka kununua betri ya laptop?

Nyie ndiyo mnaofeli mitihani kwa kujifanya mnajua sana mwisho wa siku mnaishia kusoma off-syllabus halafu mkifeli mnalaumu Baraza la Mitihani/Wahadhiri.
 

duuuh, yaishe mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…