Ushauri jamani

myhny

Senior Member
Joined
May 27, 2014
Posts
123
Reaction score
23
Kuna dada mmoja alikuwa na mwanae alomzaa bila kuolewa kaishi nae mpaka kafika mtoto darasa la 5 .kunasiku yule dada alipotelewa na pesa yake elfu kumi haijulikani kama yule mtoto aliiba pesa ya mama ake au ilipotea tu .kamuhoji mwanae akakataa na kusema hakuchukua hiyo pesa ilikua asubuhi akamwambia nikurudi niikute hiyo pesa karudi jioni jibu lilikuwa nihilo hilo kwamba yule mtoto hakuchukua pesa .yule dada akachukua mafuta ya taa na kumwagia mwanae na kumuwasha na kiberiti akatoka .mda majirani wakasikia kerere mpaka wanafika hapo nyumbani mtoto kaisha zimia .ndo na yule dada kurudi akajifanya hajui kitu na kumpeleka mtoto hospital baada ya siku tatu mtoto kuhojiwa akasema mama kanichoma ikabidi yule dada afungwe .ushauri unakuja hapa bibi wa huyo mtoto anasema eti zilikuwa hasira na shetani wakija kumhoji tena polic aseme ni hasira ni kweli huyu mama anastahiri kufungwa ama ni hasira tu
 
Ww umeshindwa kupata jibu hapo?...kuna mambo hayahitaji ushauri.
 
huyu shetan atakoma maana lawama zote kwake

mtu akizin shetan alinipitia mwingine kaunguza mtoto eti shetan
 
hasira gani za kumuwasha mwanawe wa kumzaa moto,huyo mwanamke ana roho ya kikatili na ni mgonjwa,kichwani hayupo sawa!Anaweza amdhuru huyo mtoto wake haaminiki kuachwa nae!!
 
hasira tu ndo ujaribu kumuua mtoto wako?acha afungwe tu hasira gani hizo kwani hakuna njia nyingine za kumwadhibu mtu?ana uhakika gani kama mtoto wake ndiye aliyeiba?
 
Huyo mtoto ni wake kabisaa wa kumzaa? Kama ni wake basi atakua alijifungua kwa opereshen
 
Ni mtoto wake wa kumzaaa
 
Duu humu ndani kunawatu kazi yao kujibu vitu vya ajabu .nimeleta humu ili kupata mawazo zaidi ya watu wengine sababu bibi mtu anataka mwanae achiwe sababu ni shetani .
 
Kila kitu kimejieleza kwenye maelezo yako hakuna msamaha wa kupitia neno "hasira" na "shetani" ktk sheria....huo unyama uliopitiliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…