Ushauri jamani naisi mimeshindwa

mtoto wa maskini

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
1,152
Reaction score
638
Nipo kwenye ndoa miaka 5 sasa ila mke wangu yupo Bukoba kikazi nami nipo Dar kikazi kwa miaka 3 sasa nimekuwa naonana na wife mara moja kwa mwaka yani kipindi cha likizo tu tena mwezi wa 12 siku 28 tu, sasa naisi kama nimeshindwa kuishi ivi inakuwa kama sijaoa kwa kweli, mambo yote yapo vizuri ila shida inakuja kuna kipindi mimi kama mwanaume na kuwa na hamu na tendo la ndoa na yeye hayupo inanipa tabu sana ili swala. Mana nimejaribu kuwa busy kwq kufanya mazoezi nimejaribu kuwa napiga masta ila inatuliza kwa muda tu yani inakuwa temporary solve tu, na kwa nature ya kazi zetu haiwezekani tukaamishwa kikazi tukawa pamoja, naomba kama kuna mtu ana tatizo kama langu na alifanikiwa ku solve anipe hiyo njia nitumie
 
Subiri waje mkuu,lazima wapo watu wanaokabiliana na changamoto kama zako,vuta subira wengine watoke kanisani.
 
Mmoja kati yenu amfuate mwenzie

Au likizo zeny zipangeni kila baada ya miezi 4 mchukue kwa kupokezana siku 7

Au mmoja atafute kazi ambayo atahamia kwa mwenzie

Au mfungue biashara ikitengemaa mmoja aache kazi ahamie kusimamia biashara huku mkiwa karibu
 
Hapo lazima mmoja ahame LA sivyo Luna siku kitatokea kitu cha ajabu wala hautaamin. Kuna jamaa angu yupo katika Hali hiyo ila sasa yeye amekua player balaa kama hajaoa
 
Mm pia niko Bukoba kikazi nitumie namba ya mke wako kwa ushauri zaidi
 
Yani wakati we unavumilia na kufanya ngono zembe na sabuni, wanaume wenzako huko BK wanakusaidia kumpeleka gulioni Katerero mkeo.

Kama unadhani masihara chunguza vizuri sura za wanao.

Baba ni kichwa cha familia. Toa amri mkeo aache kazi akufuate. We utamtunza kama wajibu wako unavyotaka wakati yeye akitafuta kazi nyingine kama ni lazima afanye kazi. Distance relationship haiwork. Unakaa mbali na wife kwa miezi 11 kwa mwaka??? Kwanini ulioa sasa??

Kiongozi stuka... unamegewa. Si unaona wewe unavyotaabika wakati mwenzio katulia?
 
Ndo maana tumeruhusiwa "mathna(2) wa Thulatha(3) wa Rubaa(4) !!! ili uishi hapa dunia pembezoni na ktk mazingira yoyote !!
Kila la heri !!
 

kilichopo hapa ni wewe na mkeo kuona KAZI ZENU ni muhimu kuliko NDOA YENU....siku mkigundua NDOA YENU NI MUHIMU KULIKO AJIRA mtafikia maafikiano na mmoja atamfuta mwenzie na kutafuta kazi ingine.
 
Mkuu acha utani, ina maana ukisikia mkeo ana mchepuko utalaumu kweli? Wakati umechangia kwa kuruhusu distance relationship!!! Acha hizo bhana, ambia mama yoyo ikufuate dar.
 
kilichopo hapa ni wewe na mkeo kuona KAZI ZENU ni muhimu kuliko NDOA YENU....siku mkigundua NDOA YENU NI MUHIMU KULIKO AJIRA mtafikia maafikiano na mmoja atamfuta mwenzie na kutafuta kazi ingine.

Nashukuru kwa ushauri wako
 
kilichopo hapa ni wewe na mkeo kuona KAZI ZENU ni muhimu kuliko NDOA YENU....siku mkigundua NDOA YENU NI MUHIMU KULIKO AJIRA mtafikia maafikiano na mmoja atamfuta mwenzie na kutafuta kazi ingine.

I second you, Hawa Ni watu wanaothamini sana kazi kuliko familia. Kisa cha kuishi na upweke hivyo Ni nini? Yani ndani ya mwaka wanandoa mnaonana once, kwa sababu ipi haswa ya msingi? Sidhani hata Kama wanafurahia hizo hela wanazozipata
 
Mkuu acha utani, ina maana ukisikia mkeo ana mchepuko utalaumu kweli? Wakati umechangia kwa kuruhusu distance relationship!!! Acha hizo bhana, ambia mama yoyo ikufuate dar.

Naamini awezi kuwa na mchepuko kwani ni mtu wa mungu na siku zote yupo wazi kwangu ila tatizo umbali ndio naona kero kwangu na kazi amekaa miaka 3 toka amalize chuo hakupata sasa iyo kaipata ni kama bahati kwake na ina lipa vizuri
 



mkuu mambo ya familia yanahitah azungumze na mwenzie kwa busara , umakini na kwa kina maana kwa ushauri wa amri ama ubabe anaweza akaibua tatizo lingine kubwa.

wanawake ni watu wepesi sana kuelewa endapo tu utakuwa unampenda na anakuamin anaweza kukufata tuu.
 
Kama kulivyo na mizizi ya dhambi, basi kwa mahusiano umbali ni mzizi wa mivurugano ndani ya ndoa na hasa hasa likija suala la uaminifu.
 

Sawa Mwajuma.

Hujambo lakini? Sijawahi kuwa na rafiki aitwaye mwajuma. Unaonaje ukiwa wewe?
 
Mkuu kwani hizi likizo za kama siku 3 na ukaongeza 2 na weekend unapata week huwezi kwenda?
sijui kwako lakini mimi mumewangu alivyokua anasoma USA full time mimi nafanya kazi Dubai nilipata likizo hata ya siku3 naomba na simu2 zinakua 5 na weekend siku2 natapa week nzima nakwenda,wewe hapo bukoba tuu,au kuna mambo mengine zaidi ya hayo...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…