activisty
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 315
- 107
Habarini ndugu wana JF....
Naombeni ushauri wenu katika jambo hili linalonitatiza...kuna mwanaume nimekuwa nikiishi nae takribani miaka miwili sasa.
Kisheria ni kama Mume ila moyoni mwangu simuoni kama mume...baada ya kuchoshwa na Mambo yake mengi yanayoumiza moyo wangu.nimejaliwa kuzaa nae mtoto mmoja wa kiume(6 months old).
Tatizo la huyu bwana nashindwa kulielewa hata kidogo...hajawahi kwenda kwetu angalau hata kujitambulisha na anaonekana ni mtu ambaye hafikirii kwenda kutokana na maneno pamoja na matendo yake.Kwa upande wangu ni mtu ambaye nimekuwa nikienda kwao mara kwa mara na kuwachukulia nduguze kama ndugu zangu...kitu ambacho kwake hakipo kabisa.
Kadri siku zinavyozidi kwenda ule upendo niliokuwa nao juu yake unazidi kupotea kabisa na nikimuuliza ni lini ataenda kwetu ananijibu ovyo.
Wazazi wangu wamekuwa wakiniuliza kila siku kulikon?? nashindwa kuwapa jibu...niliwatumia namba zake za simu ila hapokei simu zao.
Ndugu zangu wanaJF najua nilifanya kosa kubwa maishani mwangu kuanza kuishi na mwanaume kabla ya ndoa na tena ambaye hata kwetu hawamjui.najutia sana hili kosa...ila nashindwa kufanya maamuzi yeyote sijui kwa nini huenda ni kwa vile nanuwazia sana my son.
Ninaweza kusema naishi na mwanaume asije na chembe ya aibu na asiye na fadhila hata kidogo kwa jinsi ninavyovumilia mambo yake,mara nyingine anarudi nyumbani asubuh...alipolala anajua mwenyewe na sijawahi kumuuliza.
Kipato cha kuniwezesha kumlea my son alone ninacho ila naona atakosa malezi ya baba pale nitapoamua kuondoka.
Naomben ushauri wenu wapendwa.Je ingekuwa wewe ndo mimi ungefanyaje???