Ushauri: Hataki tutumie kondom

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,204
15,198
Salaam wakuu,

Poleni na harakati za maisha.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka kadhaa.

Miaka miwili iliyopita, nilikutana na msichana mrembo ambaye ana kila sifa ya kuitwa mrembo. Ana umbo zuri, kuanzia kifuani mpaka kiunoni. Ana sura nzuri na ya kupendeza ambaye humlazimu kila mwanaume kumtazama mara mbilimbili kila amtazamapo.

Ana tabia nzuri na inayokubalika na jamii. Mwisho ni kipanga, yupo vizuri sana darasani na ana malengo mazuri ya kuwa daktari bingwa wa moyo. Kiukweli anapendeza na kila mwanaume angetamani kuwa naye.

Baada ya mawasiliano kati yetu, kama kawaida mwanaume nikatia maneno kwa mtoto mzuri ambaye siyo tu nilimpenda lakini nilitamani sana awe nami. Japo alionekana kukataa lakini mwishowe alikubaliana na tukawa wapenzi.

Nilimpenda sana huyu binti na bila shaka alinipenda barabara. Ukaribu wa wilaya zetu ulinipa mwanya zaidi wa kumfatilia mienendo yake na zaidi kuifahamu familia yake. Hakuwahi kunificha chochote nilichohitaji kumjua na aliniambia vingi isipokuwa siyo vyote.

Katika ufatiliaji wangu, nilikuja kusikia fununu kwamba babaye ni muathirika wa gonjwa hili matata (UKIMWI). Na iliniwia ugumu kumuuliza lakini baadae nilijikaza kiume na kumuuliza endapo hizo story zina ukweli ndani yake.

Kiukweli wala hakunificha chochote, alinambia kila kitu bila kusita kuwa babaye ni mgonjwa na alipata hayo maradhi lakini mamaye ni mzima kabisa. Yeye alizaliwa kabla ya baba yake kutwaa hayo maradhi.

Ndiyo, niliendelea kuhangaika kumjua zaidi. Nilikuja kusikia ya kwamba, binti pia ni mgonjwa. Nilipomuuliza, hata hakutetereka aliniuliza "je ijapo mama yangu ni mzima, mimi nitakuwaje mgonjwa?" Nilijipatia jibu ya kwamba alimaanisha hakuwa mgonjwa hata chembe.

Sikuchoka kutaka kumfahamu zaidi. Mimi nilikuwa nasoma shule ya wavulana tu na yeye shule ya wasichana tu hivyo shule zetu kualikana kwenye sherehe ilikuwa ni kitu cha kawaida kabisa.

Nilipata kuwajua marafiki zake wengi naye aluwafahamu upande wangu. Baadae,nikaona nihamishie uchunguzi wangu shuleni. Nilichonga dili na rafiki wake wa karibu sana,na alikuwa akinipa kila habari zote muhimu ambazo tulikubaliana.

Nilimuuliza rafiki yake ajaribu kumchunguza sana amjue kama anatumia vidonge vyovyote. Ndiyo, kazi ilifanyika kwa ufasaha zaidi na CIA wangu alinambia kwamba hakuwa akitumia vidonge vyovyote.

Aliendelea kuwa binti huugua mara kwa mara na zaidi ni kuharisha na homa kali. Aliniambia pia UTI humsumbua sana. Mara nyingine binti hudhoofika sana lakini baadae hali yake hurudi katika hali ya kawaida.

Majibu hayo yalinitia shaka lakini upendo wangu kwa binti uliendelea kushamiri zaidi. Nilimpenda mara dufu. Siku nikikutana naye wakati amekonda, nikimuuliza mbona umekonda ghafla? Hunijibu kuwa ni msuli umekuwa mgumu kutokana na uhalisia wa combination yenyewe.

Kama wapenzi hatukuacha kufanya yale yote ya kimahaba isipokuwa hatujawahi kukutana kimwili. Ni maridhiano yetu kuwa miezi kadhaa ijayo tutafanya hivyo.

Binti hunihakikishia kwamba yeye ni bikira na nikigundua kwamba sivyo nimfanye chochote nitakachoona kinamfaa. Nauthamini sana usichana wake (bikra) lakini haikuwa sababu ya mimi kumpenda lakini imekua chachu ya kumpenda mara dufu.

Sasa, alipokuwa anarudi shuleni,pamoja na mengi tuliyoongea lakini pia tulikumbushana kuhusu ahadi yetu mwezi Mei.Tuliongea mengi ikiwa itafanyikia wapi na mengine mengi.

Tulikubaliana pia kwamba tujihadhari asije kupata mimba na njia sahihi ya kuepusha hayo yasitokee. Mimi niliona utumiaji wa kondom ungekuwa mzuri zaidi lakini mwenzangu alilikataa na kulipinga kuwa kondom ni kwa ajili Malaya. Alisisitiza kuwa utumiaji wa vidonge ungekuwa mzuri na salama zaidi na ziada yake wote tungefurahia tendo.

Sikutaka kumbishia,nilikubaliana naye. Lakini wazo lake lilinipa wasiwasi zaidi. Nilianza kujiuliza maswali mengi yenye majibu lakini yasiyo na hitimisho.

Je, Huenda ana gonjwa na anataka kunimalizia hapo? Au, ana nia ya dhati kabisa kunipa utamu wa tendo bila kondom kwa kuniamini zaidi?

Je, Nimuambie tukapime? Nikimuambia tukapime bila shaka atajua simuamini na namuhofia na hata ikagundulika hana, imani yake kwangu itakuwa ishapungua.

Je, Akikutwa nao kwasababu nimemuambia tukapime, si itakuwa mwisho wa hustle zake? Kwamba hatatia nguvu nyingi tena katika kutimiza ndoto zake. Pia anaweza kupata stroke na huenda ukawa mwisho wake.

Je, Nimwache? Ikitokea nimemuacha na baadae nikajua kwamba hakuwa ameathirika, si nitajilaumu mno? Je, Nikimuacha alafu baadae aje kujua kuwa nimemuacha kwasababu nimehisi ana ngomaatajisikiaje?

Je, Nijitoe ufahamu nivunje naye amri ya 6? Ikitokea anao je?

Binti nampenda sana naye ananipenda mno.

NAOMBENI USHAURI WENU NIFANYAJE WAKUU WANGU.

SHUKRANI NA MBARIKIWE
 
huku tunawabutua madada poa kavu kavu wewe chuma hicho unataka ukionje kwa mpira jilipue babu...ajali nyingi sio hiyo tu
Ni kweli mkuu lakini ikitokea anao si nitaukwaa? Mkuu kiukweli sipendi hilo litokee!
 
BansenBurner said:
Mwambie unahisi umeungua unaogopa kumwambukiza yy ucheki reaction yake anaweza akakupa jibu hata mimi ninao nilkua nakuficha tu.
Jibu murua kabisa. Najaribu kujiuliza,endapo hatakuwa nao na kutokubali kwenda kupima? Si itakula juu yangu? Anyway,ntafanya hvyo mkuu!
 
Acha kuongozwa na mihemko ya viungo vya uzazi.
Kujua afya zenu ni muhim sana na zingatia safari yako bado ni ndefu sana
 
Ndugu afya Ni bora Sana em kapimeni afya zenu mjiwekee uhakika zaidi usiangalie yeye ataonaje jiangalie wewe umri na afya yako usije juta huko mbele kumbe kalikua kamistake kadogo kutopima.....na hata ukijua kwa mfano ameathirika usimuache mtie moyo halafu usipende kufukunyua Sana ukiyatafta yasiokuhusu utakumbana na yanayokukera kapimeni aogope asiogope hakuna namna chukua tahadhar mapema.
 
Salaam Wakuu.
Poleni na harakati za maisha.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 20. Nasoma chuo kikuu fulani mwaka wa kwanza katika kozi ya Uhasibu.

Miaka miwili iliyopita(2014) nikiwa kidato cha 6,nilikutana na msichana mrembo ambaye ana kila sifa ya kuitwa mrembo. Ana umbo zuri,kuanzia kifuani mpaka kiunoni. Ana sura nzuri na ya kupendeza ambaye humlazimu kila mwanaume kumtazama mara mbilimbili kila amtazamapo. Ana tabia nzuri na inayokubalika na jamii. Mwisho ni kipanga,yupo vizuri Sana darasani na ana malengo mazuri ya kuwa daktari bingwa wa moyo kwa sababu anasoma PCB. Kiukweli anapendeza na kila mwanaume angetamani kuwa naye.

Nilikutana naye shuleni kwao katika mdahalo(debate) baina ya shule yetu na yao na kwa bahati nzuri tulitokea kuelewana Sana. Kizuri zaidi ni kwamba tulikuwa tukitokea katika mkoa mmoja na wilaya mbili jirani kabisa.
Baada ya mawasiliano kati yetu,kama kawaida mwanaume nikatia maneno kwa mtoto mzuri ambaye siyo tu nilimpenda lakini nilitaman Sana awe nami. Japo alionekana kukataa lakini mwishowe alikubaliana na tukawa wapenzi.

Nilimpenda sana huyu binti na bila shaka alinipenda barabara. Ukaribu wa wilaya zetu ulinipa mwanya zaidi wa kumfatilia mienendo yake na zaidi kuifahamu familia yake. Hakuwahi kunificha chochote nilichohitaji kumjua na aliniambia vingi isipokuwa siyo vyote.

Katika ufatiliaji wangu,nilikuja kusikia fununu kwamba babaye ni muathirika wa gonjwa hili matata. Na iliniwia ugumu kumuuliza lakini baadae nilijikaza kiume na kumuuliza endapo hizo story zina ukweli ndani yake. Kiukweli wala hakunificha chochote,alinambia kila kitu bila kusita kuwa babaye ni mgonjwa na alipata hayo maradhi lakini mamaye ni mzima kabisa. Yeye alizaliwa kabla ya baba yake kuutwaa hayo maradhi.

Ndiyo,niliendelea kuhangaika kumjua zaidi. Nilikuja kusikia ya kwamba,binti pia ni mgonjwa. Nilipomuuliza,hata hakutetereka aliniuliza "je ijapo mama yangu ni mzm,mimi ntakuwaje mgonjwa?" Nilijipatia jibu ya kwamba alimaanisha hakuwa mgonjwa hata chembe.

Sikuchoka kutaka kumfahamu zaidi. Mimi nilikuwa nasoma shule ya wavulana tu na yeye shule ya wasichana tu hivyo shule zetu kualikana kwenye sherehe ilikuwa ni kitu cha kawaida kabisa. Nilipata kuwajua marafiki zake wengi naye aluwafahamu upande wangu. Baadae,nikaona nihamishie uchunguzi wangu shuleni. Nilichonga dili na rafiki wake wa karibu Sana,na alikuwa akinipa kila habari zote muhimu ambazo tulikubaliana.
Nilimuuliza rafiki yake ajaribu kumchunguza Sana amjue kama anatumia vidonge vyovyote. Ndiyo,kazi ilifanyika kwa ufasaha zaidi na CIA wangu alinambia kwamba hakuwa akitumia vidonge vyovyote. Aliendelea kuwa binti huugua mara kwa mara,na zaidi n kuharisha na homa kali. Aliniambia pia UTI humsumbua sana. Mara nyingine binti hudhoofika sana lakini baadae hali yake hurudi katika hali ya kawaida.
Majibu hayo yalinitia shaka lakini upendo wangu kwa binti uliendelea kushamiri zaidi. Nilimpenda mara dufu. Siku nikikutana naye wakati amekonda,nikimuuliza mbona umekonda ghafla? Hunijibu kuwa ni msuli umekuwa mgumu kutokana na uhalisia wa combination yenyewe.

Kama wapenzi hatukuacha kufanya yale yote ya kimahaba isipokuwa hatujawahi kukutana kimwili. Ni maridhiano yetu kuwa mpaka atakapomaliza kidato cha sita May 2016 ndipo tutakapovunja amri ya 6. Binti hunihakikishia kwamba yeye ni bikira na nikigundua kwamba sivyo nimfanye chochote nitakachoona kinamfaa. Nauthamini sana usichana wake (bikra) lakini haikuwa sababu ya mm kumpenda lakini imekua chachu ya kumpenda mara dufu

Sasa,alipokuwa anarudi shuleni,pamoja na mengi tuliyoongea lakini pia tulikumbushana kuhusu ahadi yetu mwezi Mei.
Tuliongea mengi ikiwa itafanyikia wapi na mengine mengi. Tulikubaliana pia kwamba tujihadhari asije kupata mimba na njia sahihi ya kuepusha hayo yasitokee.
Mm niliona utumiaji wa kondom ungekuwa mzuri zaidi lakini mwenzangu alilikataa na kulipinga kuwa kondom ni kwa ajili Malaya. Alisisitiza kuwa utumiaji wa vidonge ungekuwa mzuri na salama zaidi na ziada yake wote tungefurahia tendo.

Sikutaka kumbishia,nilikubaliana naye. Lakini wazo lake lilinipa wasiwasi zaidi. Nilianza kujiuliza maswali mengi yenye majibu lakini yasiyo na hitimisho.

Je,huenda ana gonjwa na anataka kunimalizia hapo? Au,ana nia ya dhati kabisa kunipa utamu wa tendo bila kondom kwa kuniamini zaidi?

Je,nimuambie tukapime? Nikimuambia tukapime bila Shaka atajua simuamini na namuhofia na hata ikagundulika hana,imani yake kwangu itakuwa ishapungua.

Je,akikutwa nao kwa sababu nimemuambia tukapime,si itakuwa mwisho wa hustle zake? Kwamba hatatia nguvu nyingi tena katika kutimiza ndoto zake. Pia anaweza kupata stroke na huenda ukawa mwisho wake.

Je,nimwache? Ikitokea nimemuacha na baadae nikajua kwamba hakuwa ameathirika,si nitajilaumu mno? Je,nikimuacha alafu baadae aje kujua kuwa nimemuacha kwa sababu nimehisi ana ngoma,atajisikiaje?

Je,nijitoe ufahamu nivunje naye amri ya 6? Ikitokea anao je?
Binti nampenda Sana naye ananipenda mno.

NAOMBENI USHAURI WENU NIFANYAJE WAKUU WANGU. SHUKRANI NA MBARIKIWE
Huu sio uandishi wa kihasabu!!

Nasubiri sehemu ya pili ya hadithi hii
 
Mwambie mkapime wote kwa usalama wenu, damu ikichafuka haina spare mkuu..
 
Solution ni kupima..don't try to throw your life away in a few minutes pleasure..tena you are still young..unatakiwa ukazane na masomo..akikataa kipima au condom don't do it
 
Back
Top Bottom