Ushauri: Edward Lowassa asikanyage Arumeru, atamponza Sioi

Ushauri: Edward Lowassa asikanyage Arumeru, atamponza Sioi

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,104
Reaction score
128,726
Wanabodi,

Huu ni ushauri wangu wa bure kwa Mhe. Edward Ngoyai Lowassa kuwa japo amerejea nchini akiwa fit na yuko tayari kwa mapambano yoyote, namshauri asitumbukize mguu wake kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Arumeru ili asimponze bure Sioi.

Mimi ni miongoni wa wale wakweli wachache humu jujwaani "we take people for who they are not what they are" hivyo tunamkubali Lowassa kwa uwezo wake wa maneno machache na vitendo virefu, tofauti na wenzetu wengi humu wanaowashangilia watu wa maneno mareefu na vitendo sifuri!

Nimemshauri Mhe. Lowassa asitie mguu Arumeru kwa sababu Sioi anaweza kusimama mwenyewe na kutembea bila "walker"!, na pia anaweza kukamata kijiko na kula mwenyewe bila kuhitaji kulishwa, "spoon fed" na ba mkwe!.

Kufuatia maneno maneno ya the role of EL kwenye uchaguzi wa ndani wa CCM kulikopelekea Sioi kupitishwa, let this role end off inside CCM sasa "its high time let the people say!" tusiwasemee wana Arumeru kwa fulana, kofia na shibe ya siku moja!, Tuwaache wana Arumeru wajichagulie chaguo lao ambalo tayari walishachagua wanasubiri tuu kuthibitisha, hivyo Lowassa hana sababu kabisa hata ya kutumbukiza mguu wake ili kijana athibitishe amepata ushindi wa kishindo wa yeye kama Sioi na sio kushinda kwa kusaidiwa na ba mkwe!

Ingekuwa Sioi ni mwana CCM mwingine tuu wa kawaida asiye na nasaba yoyote na Lowassa, ningemshauri Lowassa apige kabisa kambi Arumeru, lakini kwa vile Sioi na yeye ni mtu na mkwewe, Lowassa akitia mguu Arumeru na atatibua ushindi laini wa Sioi kuonekana umepatikana kwa nguvu za ziada ambazo kiukweli hazihitajiki!.

Juzi nilifurahi kumuona EL ITV kwani sasa wamelift ile ban yao kwake, na aliposema yuko fit kwa mapambano yoyote, namshauri ahifadhi nguvu zake kutengeneza the "winning coalition" yake ndani ya uchaguzi wa ndani wa CCM ili 2015 yeye ndie apitishwe kuwa mgombea wa CCM huo ufit wake aje auonyeshe kwenye uwanja rasmi wa mapambano ya kweli ili tupate rais kutoka Kaskazini na kupata ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania!.

Naomba kuawasilisha.

Pasco
Update
Wanabodi, kushindwa kwa Sioi ni matokeo ya kuupuuza ushauri huu!

Mimi nilimtegemea Sioi ashinde kwa kura za symphathetic votes ili kumfuta machozi ya kufiwa. EL kamponza kijana kapigwa chini!

Wenye uwezo wa kunielewa naomba mnielewe, wale wengine msio na uwezo, nieleweni hivyo hivyo mnavyoelewa maana huo ndio uelewa wenu.

Pasco.
 
EL kwa siasa za jukwaani si mzuri sana, bali ni strategist mzuri. Akikaa kimya na kupanga mikakati tu impact yake itakuwa kubwa kuliko akianza siasa za kujibizana kwenye majukwaa. Personally, naona atapita njia ile ile ya BWM. (which is not good kwake binafsi, kwa SIOI wala kwa chama chake)
 
Wewe Pasco leo umepotoka, alafu kwanini unamshobokea shobokea huyu EL, anakupa nini hasa? Lazima kuna kitu nyuma kimejificha. EL mimi namuona mwizi tu wa rasirimali zetu, huyu EL namuweka katika kundi moja na Mkapa, hata wakifa kesho siwezi kuwakumbuka kwa lolote jema.
 
Mkuu Pasco Lowasa niliyemuona jana kwenye TV hayuko Fit kama alivyosema na nakuambia HAWEZI hata kusimama Jukwaani kwa Dakika Ishirini lazima Aende Chini. Lowasa ni MGONJWA
 
Mkuu Mayalla inatakiwa utambue kuwa Lowassa anajua kujitetea sana, na pia yuko vizuri sana kwenye mchezo wa kuiba masanduku ya kura, kununua kadi za kupiga kura, kumleta mkenya kutawala meru, kwakweli hapa yupo vizuri. Lakini jukwaani nakuambia Lowassa ni mweupe pee!
 
Umeongea vizuri pasco , laigwanan hana haja ya kuja huku meru maana ushindi upo wazi kabisa kwa sioi .
 
sioi hashindi arumeru hata wampeleke nani! leo kwa mara ya kwanza nimemuona akiongea, hafai kiukweli bora apewe nafasi ndan ya magamba na sio arumeru. huyu EL mi nshapoteza imani nae.
 
Wewe Pasco leo umepotoka, alafu kwanini unamshobokea shobokea huyu EL, anakupa nini hasa? Lazima kuna kitu nyuma kimejificha. EL mimi namuona mwizi tu wa rasirimali zetu, huyu EL namuweka katika kundi moja na Mkapa, hata wakifa kesho siwezi kuwakumbuka kwa lolote jema.
Wewe fara tuww
 
Nahisi hii thread ni mahsusi kuchota maoni ya watu kama EL aende au asiende Arumeru Mashariki. Wazo la nani?
 
Nacho kiona hapa ni kwamba Lowasa anataka kuvuga ndoa ya binti yake. Alafu na yeye ataenda aseme Sioi ni Mwanamme wa Shoka? toba!!
 
Lowassa inabidi aende Arumeru ili awadhihirishie wafitini wake kuwa yeye ni next level katika uwanja wa siasa. Anatakiwa awe chachu [ catalyst ] ya kupelekea ushindi wa kimbunga kwa Siyoi. Atawaziba mdomo wanafiki wanaodhani Lowassa si chaguo la umma 2015.
 
Wewe Pasco leo umepotoka, alafu kwanini unamshobokea shobokea huyu EL, anakupa nini hasa? Lazima kuna kitu nyuma kimejificha. EL mimi namuona mwizi tu wa rasirimali zetu, huyu EL namuweka katika kundi moja na Mkapa, hata wakifa kesho siwezi kuwakumbuka kwa lolote jema.

duuuuuhhh
 
Yatamkuta ya mkapa mwache aende aone, kwani wakati baba wa taifa wanamuua yeye alikuwa nani tena!
 
Wewe Pasco leo umepotoka, alafu kwanini unamshobokea shobokea huyu EL, anakupa nini hasa? Lazima kuna kitu nyuma kimejificha. EL mimi namuona mwizi tu wa rasirimali zetu, huyu EL namuweka katika kundi moja na Mkapa, hata wakifa kesho siwezi kuwakumbuka kwa lolote jema.
Mkuu nashukuru umenisemea kila kitu juu ya huyu bwana maana unafiki unamsumbua
 
hata km ni m w z lkn ni mchapa kazi kuliko mp.

Kazi anayoichapa ni kuiba, hatuhitaji wezi, hatuhitaji mtu hodari na jasiri wa kutengeneza mitandao ya wizi!!!!! naamini mnatafuta kuelewa sababu ya waarabu kujitoa muhanga.
 
Back
Top Bottom