Ushauri: Chaguzi zote za marudio zisimamishwe, zisubiri bajeti ya uchaguzi 2020

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Wanabodi, mimi kama Mtanzania,nastahili kuijenga nchi yangu bila kujali itikadi yangu kichama.

Kujenga nchi kunahitaji mambo 2; fedha na vipaumbele!

Fedha ilishatengwa ktk bajeti ya bunge la April- Juni 2018 na vipaumbele vyake.

Hii tabia ya wabunge ambao ndiyo waliopitisha hiyo bajeti kusema wanaunga mkono sana au siyo sana,si wakati wake huu. Ati naunga sana hivyo nichaguliwe mara ya pili kama nyoka anavyotoa gamba siafikiani nayo hata chembe.

Maraisi waliotangulia,walifanya makubwa sana tena bila ubaguzi huku wakiwa pamoja na wabunge wa upinzani! Hadi walikunywa chai pamoja Ikulu!

Kwa mtu ambae anaamua kuhama upande mmoja, ni swala binafsi sana,ambalo halinifanyi mimi nitoe kodi yangu zaidi kifuata wazo lake hilo!

Siafiki kabisa serikali kukosa fedha ya kukarabati barabara hapa Namtumbo ili fedha iunge mkono wazo binafsi la mtu mmoja . Hii haiji.

Kama ni uchaguzi, ulishapita 2015 na bajeti inayoandaliwa ni ya uchaguzi wa 2020 au huu wa SM 2019.

Nieleweke, sipingi maendeleo ya majimbo au juhudi za nchi kujenga uchumi imara kupitia utawala bora, bali tupime tija ya pale tunapoelekeza rasilimali zetu.
 
acha ujinga wangekuwa wanahamia chadema vipi ungekuna hapa kuweka uharo wako.bajeti yake ipo 2017/2018
Mkuu soma vizuri post yangu, mimi ni Mtanzania, kunipeleka nisiko ni mawazo yako!
 
Back
Top Bottom