USHAURI: CHADEMA Boresheni ofisi za Chama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: CHADEMA Boresheni ofisi za Chama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mshaurimkuu, Jan 25, 2011.

 1. m

  mshaurimkuu Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Viongozi na Wanachama wa Chadema na Wote Wenye Nia Njema;

  Kwanza najua mapenzi yasiyo ya kinafiki kwa chama ni kitu ambacho hakilazimishwi, bali hutoka moyoni kutokana na mchango wa chama husika kwa ukombozi na utetezi wa maslahi ya taifa na wanyonge wavuja jasho. Hivyo basi kwa kuwa mmefanikiwa sana katika hili la kutetea haki za wanyonge, ndugu zangu, mko juu pengine kuliko mnavyodhani; Chama kinapaa.

  Natambua hivi karibuni, Kada maarufu wa CCM lakini Mzalendo wa kweli, Mzee Mustapha Sabodo, bila kuangalia chama chake bali ni chama gani chenye muelekeo wa kulitetea taifa, aliwapatia mchango (msaada) kutoka katika HAZINA YA MAPATO YAKE YALIYOPATIKANA SI KWA DHULUMA BALI KWA HALALI ili kukisaidia chama chenu - CHADEMA. Na nyinyi bila ajizi mkalenga pale pale - KUJENGA CHUO CHA MAADILI YA UONGOZI - hakika haya ni maono.

  Pamoja na hayo, kwa kweli kwa hadhi ya chama ilivyo sasa, Makao yenu Makuu pale Kinondoni HAPATOSHI. Sijui Ofisi za Mikoani hadi wilayani zinafananaje, nawaombeni hili mlitilie mkazo katika vipaumbele vyenu - kabla ya uchaguzi mkuu ujao, Chama kiwe kimepata Ofisi kubwa (jengo lake yenyewe) na ya kutosha kwa ajili ya Idara zote za Chama bila kusahau Maktaba na Makumbusho ya Chama ambapo mwananchi yeyote atakuwa huru kutembelea na kupata taarifa mbali mbali za Chama na Nchi na si kucheza bao, kutafuna kashata, au kutembeza umbea na majungu kama kule kwa wenzenu.

  Hela zitatoka wapi? Najua hamna vitegauchumi kwani hamkopora rasilimali za taifa kama viwanja vya mipira, majengo, n.k. wala hamna EPA, Meremeta, DOWANS, n.k lakini MIOYO ya WAZALENDO ni hazina kuu kuliko yote hayo. Hamasisheni wananchi (sio mafisadi) wawachangie muone mambo - ni suala la organaizesheni na maono tu. Hivyo viruzuku vitumike kwa masula mengine, lakini masuala mazito ya Chama tuleteeni sisi wananchi; tuko nanyi daima.

  Nawasilisha hoja.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  mimi sikuungi mkono.jambo la muhim ni CDM wazidi kuboresha rasilimali watu na IT TECHNICIANS na sio majengo wa makao makuu,
   
 3. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  nakuunga mkono,Hii muhimu. Ila iendelee sambamba na vipaumbele vingine vya kisera na mapinduzi
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Pale ilipo inatosha sana... after all ofisi inatakiwa ya mtendaji mkuu tu yaani katibu mkuu na sehemu ya kutunzia documents za ofisi hivyo pale panatosha!!!
   
 5. m

  mshaurimkuu Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Samahani;

  Naomba kuongezea, pamoja na rasilimali watu na IT, pia hakikisheni mnafungua KITUO CHA REDIO (FM) haraka iwezekenavyo. TV na gazeti rasmi la Chama vinaweza kufuata baadaye. Tuleteeni mapendekezo yenu, msikae kimya ilhali wananchi tupo. Mbona ile mijizi inavyo na huvitumia vibaya kumwaga sumu mbaya kwa umma? Sasa tunahitaji vitakavyoondoa sumu na kuuelimisha umma.
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  kwi kwi kwi kwi,
  Viongozi wepi hao watayofanya hayo? wa CHADEMA aah wapi nakataa.
   
 7. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  TV na Radio on pipeline.

  Ofisi za chama zitaendana pamoja na chuo cha maadili. Tayari yanafanyiwa kazi!

  Hongera kwa kuwa na maono hayo. Viongozi tayari wameshaanza na tutafanikiwa. Rasilimali watu pia.

  Ofisi za mikoani na wilayani ni muhimu sana. CDM imeliona hilo!
   
 8. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mie Nashauri kuunda mtandao mpana wa kuwafikiwa wananchi vijijini na kuwaunganisha na Viongozi wa CDM wa Kitaifa.

  Mfano, Katika Kila Kijiji Au tarafa, kuwe na kiongozi au Mwakilishi wa chadema. huyo Kiongozi au Mwakilishi inatakiwa ajulikane au atambulishwe kwenye mkutano wa Hadhara na atoe namba zake za simu. Hivyo kupitia yeye atawaunganisha na Viongozi wa juu makao makuu, mkoa, mbunge kama yupo, na wilaya.

  kupitia hao viongozi, wananchi wanaweza kupeleka malalamiko yao, kero au mapendekezo na hivyo kuimarisha chama cha ukombozi - CHADEMA.

  Pia itawasaidia wananchi kutatuliwa matatizo yao yanayotokana na Viongozi wa Serikali iliyopo madarakani. mfano masuala ya ardhi, michango mashuleni n.k ambayo ni kero kubwa. Masuala ya kisheria pia wananchi wanaweza kusaidiwa.
   
 9. m

  mshaurimkuu Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  In fact pamoja na kuwafikia wananchi, inatakiwa pia kuanza kuandaa mawakala kwa ajili ya 2015 sasa badala ya kusubiri karibu na uchagunzi mkuu ambapo mnaweza kuingiza makapi mengi kama maandalizi hatafanyika mapema na vizuri.

  Pamoja na matarajio makubwa kwamba huenda Katiba mpya inawezekana ikapatikana kabla ya uchaguzi hivyo mambo baadhi ya yakabadilika ikiwepo 'TUME YA UCHAGUZI', kwa mfumo wa nchi hii, hilo laweza pia lisiwezekane na mambo yakawa yale yale; hivyo ni muhimu KUJIANDAA KWA LOLOTE.
   
 10. F

  Fenento JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimependa mambo mawili, kwanza thread yenyewe ni nzuri sana katika kuhakikisha tunaboresha mambo ya ofisi pamoja na masuala mengine yanayohusu chama.

  Pili nimependa maelezo ya Mkuu Alberto kwa kutujulisha kuwa mambo yanaenda vizuri na viongozi wetu wa CDM wanayafanyia kazi. Tunaomba sana wenzetu ambao ni viongozi au mpo karibu na viongozi kufikisha hii michango ya mawazo kwa viongozi pamoja na kutupa majibu kama bwana Alberto alivyofanya.

  Feedback ni muhimu sana kwavile wengine tupo mbali lakini tutajua mambo yanavyoendelea huko kwa lengo la kulikomboa taifa letu kutoka kwenye ukoloni wa viongozi wetu ambao kwa muda wote wameshindwa kuwatumikia watanzania.
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kitengo cha mawasiliano Chadema makao makuu kiimarishwe kwa kuajiri wataalamu na wenye kauli rafiki. Kuna watu wanajitolea mambo mengi sana na nguvukazi katika maeneo yao lakini wanapokuja makao makuu kwa ushauri na utekelezaji wanavunjwa moyo na majibu na mwiitikio wa wahusika. Hii imegarimu sana chama tangu wakati wa Uchaguzi, na inaonekana haijafanyiwa kazi.

  Upatikanaji wa vifaa nao ni tatizo lingine kubwa. Kuna urasimu kuliko serikalini, nobody seem to care. Wengine wanauza official materials na wengine wanagawa bure. It is chaotic and discouraging kwa wananchi wanaojitolea nguvu na muda wao kuanzisha matawi ya chama maeneo yao
   
Loading...