Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,325
- 152,136
Kwa kuwa vituo binafsi vimeruhusiwa kurusha matangazo ya Bunge live, nawashauri CHADEMA waanzishe harambee na pia kuomba wafadhili wa chama wawasaidie katika kuanzisha kituo chao cha Tv ambacho kitaendeshwa kibiashara na pia kitatangaza shughuli za Bunge moja kwa moja.
Kituo hicho pia kitawasaidia katika kampeni za mwaka 2020 kama jinsi Star tv ilivyowasaidia CCM katika kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.
Mna muda wa kutosha mpaka 2020 na mnaweza kuanza na mikoa michache kwanza.Hatua hii itakuwa ni ushindi mkubwa kwenu kisiasa na pigo kwa wabaya wenu labda tu wawafanyie mizengwe katika kuwapa leseni au kurusha matangazo hayo live.