Asante sana kwa mawazo haya. Hakika yamenijenga sana. Mungu akubariki.Naona mtanganyika amekujibu vizuri sana lakini sio mbaya na mimi nikiongeza machache. Mkuu hizo formula ambazo washindani wako wanatumia kutengeneza bidhaa zao kwenye lugha ya kisheria ndio hati miliki(Intellectual property) ambayo kiundani zaidi ni trade secrets, ambapo kiukweli lazima walinde siri hizo la sivyo kila mtu anaweza kuchukua ujuzi wao na kuzalisha bidhaa kama zao.
Binafsi ningekushauri kuanzia kufanya research yako google ili uone watu wengine huko duniani wanafanyaje, kama ikishindikana kupata hiyo taarifa unayoitaka huko google basi jaribu kununua izo taarifa kutoka kwa washindani wako.
Shukurani nyingi zikufikia wewe na wadau wengine kwa msaada huu wa mawazo. Tafadhali usinichoke kama nitakutaka msaada wa mawazo au ombi katika kushirikiana. Haya bado ni mawazo tu na ndio mwanzo wa mchakato, nikiwa tayari nitagonga mlango.Mkuu hapa njia moja kubwa ni wewe kuumiza kichwa kumkamata mmoja wa wazalishaji akubali kukupa mpango mzima. Na dawa ni moja tuu mlungula au cash, lakini usiende kienyeji enyeji utapoteza pesa na hupati recipe. Cha kufanya kwanza poteza muda kuisoma business yenyewe kwa nje nje macro analysis, angalia washindani wako, angalia weakness (udhaifu) wa product zote kwenye soko, angalia kama ukipata hiyo secret source utajiposition vipi kukamata % ya soko. Wakati ushapoteza muda huo na kwamba umehakiki unafahamu soko lote na umejua udhaifu wa product zilizo sokoni, sasa weka mkakati (strategy) wa kutafuta dhaifu mzalishaji (weaker) ambae atakubaliana na wewe either wa kupartner na wewe sababu unakuja na cash and technical know-how ya kuingia sokoni, au umnunue mtu kabisa wewe utengeneze mchakato mzima.
Mafuta ya nywele mimi pia natolea macho, hasa ambayo ni natural ingredients yasiyo na artificial chemicals. Kingine sababuni za kuogea na shampoo vyote liquid hii nayo naitolea macho.
Ni vema kama tungekuwa tunaorodhesha mada kadhaa na kuanza kuchambua mojamoja kwa kina kuliko kugusa juujuu.
Sh
Shukurani nyingi zikufikia wewe na wadau wengine kwa msaada huu wa mawazo. Tafadhali usinichoke kama nitakutaka msaada wa mawazo au ombi katika kushirikiana. Haya bado ni mawazo tu na ndio mwanzo wa mchakato, nikiwa tayari nitagonga mlango.
Kaka ninakusoma sana yaani kama upo kwenye akili yangu teh teh tehUnajipangaje kutoka ujasilimali mdogo kwenda wa kati? Tupo mchakato wako, nini unafanya kukutofautisha na vida umiza vyote vya stationary kila kona. Nikupe idea moja, anzisha customer list ( horodha ya wateja wako), kila mteja atakae kubali kuweka jina kwenye list yako unamuwekea lengo kwamba ukipiga copy 100 ndani ya mwezi huu basi kwa miezi 2 ijayo nakupa 10% punguzo, hii itakuongezea wateja na royalty ambayo ndio kitu muhimu zaidi