Mtanganyika
JF-Expert Member
- Jul 18, 2007
- 1,601
- 951
Wakuu,
1. Fahamu Biashara Yako Nje Ndani
Muda kama huu kama huifahamu biashara yako kindakidaki utakwenda na maji tuu. Unakutana na mtu anakwambia nina biashara yangu ya butcher, unamuliiza kwa siku unazua kilo ngapi anakwambia kuna siku nauza 60KG siku nyingine 45KG, unatamani umkate makofi sababu hajui anauza KG ngapi. Anajua inabidi akwambie kwa wastani nauza 55KG kwa siku, ndani ya mwezi huu mauzo ya juu ya siku yalikuwa 75KG na mauzo ya chini yalikuwa 45KG, faida yangu ni 40% ya bei ninayo nunulia ambayo ni xxx kwa siku napata faida ya shiling kadhaa kabla ya kutoa gharama za undeshaji kadhaa.
Umeona mtu anaejua anachofanya na anae subiri speed ya mwendokasi imtoe njiani. Lakini ukiachilia kufahamu financial zako, lakini lazima ufahamu wateja wako. Unatakiwa kujua jee unawateja wangapi ambao wanarudia rudia kufanya biashara na wewe na jee unawapa nafasi ya kwanza? Jee wateja wangapi wapya unapata kwa week? kwa kila mteja mmoja anatumia kiasi gani katika biashara yako? Jee una mpango wa kuwapa wateja motisha ili waongeze ununuzi kwako.
2. Weka Malengo Katika Biashara Yako
Biashara nyingi ndogo zinaendeshwa ovyo ovyo, mtu anamkaa asubuhi anafungua jioni anafunga, akiletewa kitu na supplier hata kama hajui kitauzika yeye ananunua tuu basi ili mradi yupo yupo, ndugu yangu na mwendo kasi huu utakwenda tuu. Muhimu kujiwekea malengo, lengo kuu namba moja biashara lazima iwe na BUDGET ndio bajeti, lazima undengeneze budget ya mwezi hadi mwezi ambayo mwisho ikupe budget ya mwaka. Katika budget yako ya mwezi lazima uweke makadirio ya mauzo kwa mwezi, makadirio ya gharama na makadirio ya faida. Makadirio ya mauzo lazima yawe yanaongezeka kwa kiasi fulani, na nilazima uweke mchakato wa kusukuma mauzo yako kufikia makadirio. Mwisho wa siku ni muhimu kulinganisha makadirio na mauzo, na kuelezea tofauti yoyote iwe ya juu au chini.
Mfano; una duka la hardware, umebudget mauzo kuwa 100 na mwisho wa mwezi yakuwa 90 lazima uwe na mchanganuo kwa nini budget yako imekuwa 10% below. Vilevile wanaokusaidia katika biashara lazima wote wafahamu malengo ya kila mwezi na mwaka ni mkakati wa kufikia malengo.
2. Boresha Huduma Kwa Wateja
Ushindaji wa biashara umeongezeka sana na hali ngumu ya maisha inapamba moto. Sasa kama utaamua kufumbia macho kuweka mkakati wa kuwajali wateja basi mwendo kasi lazima likutoe njiani. Mkakati wa kuwajali wateja lazima uandikwe chini, sio kusema tuu nina wajali wateja. Hapana tengeneza hata kurasa mbili za mkakati wa kuwajali wateja, fundisha wafanyakazi wako wote mkakati huo, haijalishi mfanyakazi wa uwani au offisini, wote lazima wafahamu mbinu za biashara yako ya kuwajali wateja. Ushasikia neno mteja mfalme, wengi tunadhani lile neno ni usemi tuu, hapana ukimuhundumia mteja kama mfalme ujue atarudi tuu.
Weka mkakati wa jinsi ya kuwajali wateja wako, wafundishe wafanyakazi wako. Hakikisha kila saa una sura ya kutabasamu, tumia maneno kama tafadhali, karibu. Kama kitu hicho huna mwambie kwa ukimya kwa nini huna, zungumza na mteja ukiwa umeacha kila kitu, sio unaongea na mteja huku upo kwenye Instagram. Weka kisanduku cha kuwauliza wateja wanaonaje huduma yenu, chukua takwimu, fanya improvement kwenye mapungukufu, toa motisha kwa wafanyakazi wenye kujali wateja kwa hali ya juu.
Wakuu hizo ni moja dondoo chache ambazo zinaweza kusaidia biashara yako ikakuwa kwa speed ya juu wakati huu mgumu.
Nilipotea kidogo, sasa nimerudi. Nakamilisha usajili wa kampuni yangu itakayo julikana kama Faru Venture Capital (FVC), lengo ni kuwekeza kwenye biashara zenye uhitaji wa mitaji midogo na ya kati, kwa kushirikiana. Muda ukifika nitalizungumzia zaidia.