BenKaile
JF-Expert Member
- Oct 17, 2014
- 443
- 376
Nimepata wazo leo wakati tukiwa tumejumuika vijana kikundi kidogo cha wakazi wa K-Nyama, tukizungumza na kupeana ushauri kuhusu maswala ya ndoa na nimeona nishirikishe moja ya ushauri wangu humu JF kuhusu hoja ya TALAKA kwenye familia zetu hususani nyakati hizi zenye changamoto kemkem.
Wenzi wa ndoa wanaotalikiana huwazia kwamba kufanya hivyo ni shuluhisho la kudumu kabisa, yaani, talaka yao itawaondolea kabisa huzuni na ugomvi mkali uliopo, na badala yake wapate utulivu, furaha au hauweni maradufu. Lakini kutarajia hilo ni sawa tu na kutarajia kuwa na ndoa kamilifu wakati changamoto zipo kila kukicha na hazifungamani na mtu mmoja pekee unayemuacha, haiwezekani.” Hivyo, ni muhimu kuwa na habari kamili na kuona talaka kihalisi kabla ya maamuzi sahihi.
NB; Nimelenga ushauri huu kwa wanandoa pekee (mume & mke) na sio wanandoa walioanzisha familia tayari, yaani Baba, Mama na (M)watoto.