The Hidden
JF-Expert Member
- Mar 26, 2017
- 246
- 102
Habari zenu wana JF? Kwa sasa mimi naweza sema nina ufahamu mpana sana juu ya ishu ya mahusiano kwani nilikaa katika uchumba kwa miaka kadhaa na tangu nioe sasa ni karibu miaka miwili lakini kwa hili la huyu ndugu yangu nimeshindwa kulielewa japokuwa ananitegemea mara nyingi sana katika ushauri so imebidi nikwepe kuzungumza naye juu ya hili nipate mawazo yenu kwanza:
Rafiki yangu huyu ambaye sasa ni kama ndugu, amekuwa na mahusiano na binti mmoja ambaye mpaka sasa ni miaka 2 na nusu(kwa maelezo yake) wakiwa kama wachumba binti huyu ni mvumilivu katika dhiki ya kukosa pesa na japokuwa kuna wakati wanatofautiana mara nyingi alikuwa akinishirikisha nikamshauri na wakarejeana.
Leo hii ameniijia anasema ni mara ya pili sasa amekuwa akimsikia mpenzi wake huyo(mke) ambaye anaoneshaga kuwa ni mtu mwenye wivu sana, akimwambia huyu ndugu kuwa kama atamuoa na ikatokea amemsaliti yaani kuchepuka basi atamuua abaki tu na nyumba, jamaa anasema kwa mara ya kwanza haikumuingia akilini sababu alidhani ni utani tu ila leo hii wakiwa wanaangalia movie iliyoonesha mshikaji mchepukaji alirudia tena kumwambia hivyo, hii kauli sasa imemchanganya na anajihoji amuoe au amuache huyu mwanadada.
Nimejifikiria sana kwa upande wangu nimeshindwa kumwambia jamaa nini aamue ikiwa jamaa anaonesha kumhitaji huyu mwanamke ila anahofu kauli hizo na mwanadada pia huwa anaonesha anampenda sana jamaa!
Nimejiuliza kwa upande wangu hivi inawezekana mwenye dhamira ya kufanya hivyo akajinadi kabisa? Au alitumia kauli hizo kumtishia tu jamaa asijechepuka? Na pia hayo mawazo anayatoa wapi kama si kwamba labda alimaanisha?
Karibuni wadau mnipe pa kuanzia kwasababu nimemuahidi jamaa kuongea naye juu ya hili hapo kesho