Ushauri: Amebakwa na kupata mimba, niendelee nae kweli?

Ushauri: Amebakwa na kupata mimba, niendelee nae kweli?

gambada ynwa

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2014
Posts
394
Reaction score
376
Wakuu kwema?

Kuna dada mmoja ni shemeji yangu yaani ni mpenzi wa mshikaji wangu. Wamebahatika kupata mtoto mmoja, japo walipanga wafunge ndoa mwaka huu ila kuna mambo hayakwenda poa wakaona wajipange kwanza kidogo.

Sasa huyu dada kuna siku alikua anasafiri ikabidi atafute nyumba ya wageni alale ili kesho yake aendelee na safari. Bahati mbaya hakua na pesa za kutosha hivyo akaamua atafute lodge ya bei ya chini.

Kumbe haikua na ulinzi wa kutosha. Sasa usiku akagongewa mlango na mtu aliyejitambulisha kama mhudumu na alipofungua tuu wakaingia majamaa wawili wakiwa na visu mikononi wakamtishia kumuua kama akipiga kelele, wakambaka wote wawili.

Bahati mbaya alikua kwenye siku za hatari na akashika mimba. Aliwaza kuitoa ila doctor akamshauri aache maana ana matatizo ya presha.

Sasa wakuu huyu dada ni kama amechanganyikiwa na anadai asingekua na huyu mtoto wake angejiua. Ila anashindwa maana mtoto wake anamtegemea.
Sasa huyu mshikaji wangu nae kachanganyikiwa afanye nini.

Wakuu mtu kama huyu namshauri vipi?
 
Mkaka alee mimba ya mpenz wake na Dada atulie na mimba kwan hakufanya kusud kupata hyo kitu
 
Huyo dada atoe maelezo ya kueleweka tu. Alikuwa targeted yeye au lodge ilikuwa imevamiwa?! Hawa dada zetu siku hizi ujanjaujanja mwingi hasa for the sake of marriage.
 
Kwa vile imetokea bahati mbaya. Basi wakae chini wayamalize... japo itakuwa ngumu. Lakin ndio inavyo takiwa
 
Hata kama hii story ni ya kweli huyo daktari hewa aliyeshindwa kurecommend dawa kama p2 alikua ana hamu tu aone ugomvi wa wanandoa utafika wapi, halafu haujasema kama alihudumiwa kama ile rape kit inavyotaka.

Na hilo swala siyo la kujiuliza aendelee na mpenzi wake na kwenye ndoa mtualike.
 
Hawa wanawake sio wa kuamin nyie mlidhibitisha kabakwa kweli?au taarifa aliwapatia yey mwenyewe,maybe mimba ya mchepuko imeingia bahati mbaya,yaani hainingii hakilini eti majamaa yaliimvamia gest hao jamaa walijuaje kile chumba? maana vipo vingi vyumba aisee hilo swala liundiwe tume ya uchunguzi jamaa yako asilee mimba sio yake,hawa wanawake wakiona mambo safi ni ving'ang'anizi sana ndoa,hata alikua na basha wake wanamalengo mazuri tu kama hana pesa wanamuacha,don't trust women
 
Wazee wa zamani walikuwa na usemi kuwa kitanda hakizai haramu na mtoto ni baraka...Jamaa inatakiwa ajiridhishe kweli kama huyo mwanamke alibakwa either kwa kwenda kuulizia hapo Guest kama kuna tukio kama hilo lilitokea...Na kama ni kweli huyo mwanamke alibakwa inabidi huyo jamaa awe karibu sana na huyo mwanamke tena namna huo ujauzito ulivyopatikana iwe siri yao tu ili mtoto akizaliwa amlee na kumtunza kama wake.....
 
Back
Top Bottom