USHAURI: Achague yupi kati ya wawili hawa?

chungutamu

Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
13
Reaction score
3
Habari wana Jf?

Wapendwa, nina rafiki yangu anahitaji ushauri la kufanya na maamuzi ya kuchukua.

Yeye ni binti na alikuwa na boyfriend wake ambae walidumu nae takriban miaka mitatu. Wakati wapo katika hayo mahusiano huyu mtu wake alikuwa na tabia ya kum cheat mwenzie na akim baini anombwa msamaha yanaisha. Hii tabia iliendelea ya huyo boyfriend wake kumsaliti hadi pale huyo dada alipoamua kuachana naye sababu ya kuto muamini tena. Hivyo akamwambia kuwa anaomba kila mtu ashike 50 zake.

Baada ya hapo rafiki yangu huyo alijiingiza katika mahusiano mengine yaliyodumu miezi 8 na wakapendana sana. Ikumbukwe kuwa Boyfriend wake wa mwanzo bado anampenda sana huyo dada. Pia kuna tatizo lililopo kwa huyu wa sasa kuwa ni tofauti ya kiimani. Mwanaume ni Muislam na hali mwanamke ni Mkristo na hataki kubadili dini, huyo boyfriend wake wa sasa amemwambia huyo dadad ole wake arudi kwa mpenzi wake wa mwanzo atahakikisha wanamkosa wote.

Je afanyeje?
 
Kwa hiyo kauli ya mwisho..hakuna mapenzi hata kwa huyo wa pili.. Kama Mtu unampenda huwezi kumtishia kumuua.. Ushauri subiri Mtu mwingine hata akiwa Dini nyingine kwani Mapenzi hayana Dini .. Ila Sisi wanadamu ndio tuna-complicate mambo...Good Luck!
 
thanks, but kuhusu hiyo kaur ya mwisho amemaanisha kua atamtaarifu yule wa mwanzo kua yy ndie alie sababisha waachane ili na yule asimpende tena kisa amekataa kua muislam
 
I see.. Lakini still sioni mapenzi ya kweli kwa huyo wa pili.. Ampotezee tu..
 
Mmmh! Udini huo, hapo mapenz ya kweli hamna kabisa, huyo dada auskilze moyo wake unapopenda ili awe na furaha coz hata huyo bf wa pili akisema hayo maneno ya uongo kama kwel jama wa mwanzo anampenda hawaz yaskliza
 
Aolewe tu kiserikali, huyo wa mwanzo hakumpenda maana asingecheat kil mara.
 
simple sana amuache halafu aone atamfanya nini cha kuuliwa nini kisa demu ndio uue mtu mwambie amwache kabisaa ni ungese anamletea bidada wa watu.. BTW mpe pole zake kwa kubug..
 
asante sana mkuu, na nikwel huyo wa mwanzo ameonyesha kumpenda sana na si yy tu had familia yake maana mama wa bf wa kwanza bado anampigia sim mpaka leo na kumsihi amsamehe mwanae
 
bidada kamshaur ivo ila yy amekataa analazimisha abadili kabsa et watoto watakua ktk mising ipi ilihali wazaz wanamitazamo tofaut
 
Huyo wa kwanza alisema anacheat, maana yake si muaminifu na hana mapenzi ya kweli. Hivyo hata kama atamrudia bado kazi ni bure, maana ajiandae kugonganishwa na pengine kuletewa magonjwa nyumbani.

Huyo wa pili analalamikiwa kwa kuwa na imani tofauti na yeye, suala la kujiuliza, ni kuwa wakati anaanza naye hakujua kama wana imani tofauti? Cha msingi akaye naye chini waangalie taratibu za kumaliza mambo hayo ya kiimani, maana imani kwa sasa ni suala lenye changamoto sana na inaweza kuigawa familia yake.

Ushauri wa bure kama huyu wa pili watashindwa kufikia maelewano kwenye suala la imani, ni bora kuachana nao wote kuliko kurudi kwa mtu ambaye anacheat kila siku. Huyo ni m-baya zaidi maana anaweza kumsababishia mauti wakati wowote. Mwambie atafute mwingine tofauti na hao. This time awe makini na kuangalia yale mambo muhimu kama imani na tabia ili asijipotezee muda wake kwa kuinvest sehemu isiyo na faida.
 
asante sana mkuu, na nikwel huyo wa mwanzo ameonyesha kumpenda sana na si yy tu had familia yake maana mama wa bf wa kwanza bado anampigia sim mpaka leo na kumsihi amsamehe mwanae

kama ni hivyo warudiane tu mkuu. Wish them ol the best
 
simple sana amuache halafu aone atamfanya nini cha kuuliwa nini kisa demu ndio uue mtu mwambie amwache kabisaa ni ungese anamletea bidada wa watu.. BTW mpe pole zake kwa kubug..

mkuu hapo kwenye kumkosa sio kwa kumuua ila kwa kumharibia kwa bf wa kwanza eti anaona wivu coz na yy bado anampenda sana
 
Shukrani Tulizo na HorsePower... Naunga mkono mawazo yenu. Lingine ambalo inabidi mhuiska atambue ni kuwa siyo lazima awe na mpenzi. Anaweza kutumia nafasi hii kuwa single na kutafakari what is best for her. Siyo lazima achague kati ya hao wawili hali ni dhahiri wote hawamfai... Anaweza wapotezea wote.

Mleta mada kama hutajali tafadhali siku nyingine andika kwa lugha iliyokamilika, umeweka vifupi mno kana kwamba unatuma message. Hapa kuna members wa kila rika. Kila la kheri katika utatuzi wa suala hili.
 
Last edited by a moderator:
Pole,

Watu wanachukulia kiutani swala la utofauti wa imani, Kuna ndoa nyingi zina migogoro ambayo inatokana na utofauti wa dhehebu tu achilia mbali utofauti wa dini. Unakuta mume ni dhehebu hili na mke ni lingine na wote ni wakristo hawa lakini ni ugomvi usioisha kuhusiana na imani zao, imagine wote ni wakristo (RC vs Lutheran vs Pentecote Vs Kakobe vs Mwingira vs Rwakatare vs Mzee wa upako etc etc you name them). Je ingekuwa na DINI zao ni tofauti, si matatizo zaidi?

Dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu kwa hiyo sio shida kuhama, shida ipo kwenye kuikana KWELI ambayo ni Neno la Mungu nalo ni Kristo.

Swala la Dini ni lina umuhimu sana kuliangalia kwa faida ya wote. Either mmoja amfuate mwingine au muachane. Hata maandiko yanasema msifungwe nira na wasio amini.
 
nashukuru sana mkuu,
 
shukran mkuu Tized
 
asante sana mkuu, na nikwel huyo wa mwanzo ameonyesha kumpenda sana na si yy tu had familia yake maana mama wa bf wa kwanza bado anampigia sim mpaka leo na kumsihi amsamehe mwanae

Kwani mama mkwe ndo ataishi nae.....tulizana dada,,,,achana na wote muombe Mungu akupe mume mwema.....
 
Pole,

Watu wanachukulia kiutani swala la utofauti wa imani, Kuna ndoa nyingi zina migogoro ambayo inatokana na utofauti wa dhehebu tu achilia mbali utofauti wa dini. Unakuta mume ni dhehebu hili na mke ni lingine na wote ni wakristo hawa lakini ni ugomvi usioisha kuhusiana na imani zao, imagine wote ni wakristo (RC vs Lutheran vs Pentecote Vs Kakobe vs Mwingira vs Rwakatare vs Mzee wa upako etc etc you name them). Je ingekuwa na DINI zao ni tofauti, si matatizo zaidi?

Dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu kwa hiyo sio shida kuhama, shida ipo kwenye kuikana KWELI ambayo ni Neno la Mungu nalo ni Kristo.

Swala la Dini ni lina umuhimu sana kuliangalia kwa faida ya wote. Either mmoja amfuate mwingine au muachane. Hata maandiko yanasema msifungwe nira na wasio amini.

Dini ni jambo la msingi kuzingatia kabla hujaingia kwenye nira, kama tatizo la kwanza ni kukosa uaminifu nadhani kwa huyu wa pili hatalikwepa kwa msingi wa tofauti ya dini, maana dini yake itamruhusu kuoa zaidi ya mke mmoja wakati kwa dini nyingine ni kukosa uaminifu ktk ndoa.

Kama bado mapenzi yapo kwa huyo wa kwanza ambao wana imani sawa ni vema arudiane naye kwani kusamehe ni moja ya tunda la roho, maana kama Mungu asingesamehe basi peponi kungekuwa tupu. Pia mtu asiyekosa kamwe hawezi kufanya jambo jipya bali aliyekosa na kutambua.
 
Ukimwona mtu anaikana imani yake LEO kwa sababu yako, elewa kwamba IPO SIKU atakukanaa kwa sababu ya mwingine.
Thanks
 
Habari wana Jf?

Wapendwa, nina rafiki yangu anahitaji ushauri la kufanya na maamuzi ya kuchukua.

Yeye ni binti na alikuwa na boyfriend wake ambae walidumu nae takriban miaka mitatu. Wakati wapo katika hayo mahusiano huyu mtu wake alikuwa na tabia ya kum cheat mwenzie na akim baini anombwa msamaha yanaisha. Hii tabia iliendelea ya huyo boyfriend wake kumsaliti hadi pale huyo dada alipoamua kuachana naye sababu ya kuto muamini tena. Hivyo akamwambia kuwa anaomba kila mtu ashike 50 zake.

Baada ya hapo rafiki yangu huyo alijiingiza katika mahusiano mengine yaliyodumu miezi 8 na wakapendana sana. Ikumbukwe kuwa Boyfriend wake wa mwanzo bado anampenda sana huyo dada. Pia kuna tatizo lililopo kwa huyu wa sasa kuwa ni tofauti ya kiimani. Mwanaume ni Muislam na hali mwanamke ni Mkristo na hataki kubadili dini, huyo boyfriend wake wa sasa amemwambia huyo dadad ole wake arudi kwa mpenzi wake wa mwanzo atahakikisha wanamkosa wote.

Je afanyeje?

Asikilize moyo wake mwenyewe!!
 
Back
Top Bottom