usharobaro kwenye msiba

unaujua wimbo huu wa Bob Marley..
''they keep us hungry, and when u gonna get some food
ur brother ought to be ur enemy yeah
ambush in the night!
they tell us what we know, is just what they teach us
and we ar nt ignorant...''
ndo haya sasa. wazike wao,kwa gharama zao, ukereke ww mtu baki,mweh!
unaonekana kua na wivu wa utajiri wao.
 
jokes/kichekesho hapo ni nini..!!!!....,binadamu wote huzikwa kwa heshima sasa kama wewe unataka tu kumchimbia ndugu yako kama mnyama mwingine yeyeto hiyo ni wewe..kiongozi...WIVU KWANGU MWIKO...
 
Watu mnalia weeeeeeee hadi mnachoka majirani wakija kuwapa pole wanakuta mnagonga kiganja kwa vicheko hadi hawajui nani mfiwa anayestahili kupewa pole!
 
hivi nyie ndugu zetu mnapofiwa na jamaa yenu mnaamua kwenda kumuhifadhi mochwali kwa muda wa wiki mbili mpaka tatu ili mshone suti au mtengeneze t-shirt nakuweka picha ya mfiwa na mbaya zaidi mmeanza na ka mtindo ka kupeleka maiti saloon. Duh!! Mnaboa kwa kweli. Kaburi mnalijengea mnanunua na grovz kwa ajili ya kushikia tu udongo saa ya kuzika kisha kaburi linafunikwa kwa mfuniko??? huyo jamaa aliekufa anaenda kuoza tu kama mnampenda si mge endelea kuishi nae ndani kwenu?? Mazishi yenu yanaboa sana enyi wenye vijisenti uchwala.
<br />
<br />


kuna baadhi ya watu hutoa kadi za mwaliko msibani
 
Dah huu wivu jamani dah, kwanini maiti isienziwe ? , utajibeba na wivu wako acha wenye nazo wawaenzi wanaowapenda!
Wivuuuuuuuuuu! yaani mtu kufiwa halafu aonewe wivu? anachoongea Prof ni sahihi, misiba mingine hadi mnasahau na mnakwenda kazini kama kawaida ukirudi ndo unakumbuka kumbe kuna msiba jirani yangu? hadi mnaofariji mnaishiwa maneno ya faraja na kwa kwli huzuni inaisha kabisa, hii ipo hasa ndugu zangu wachaga msiba wiki mbili wanaandaa mazishi!
 
mie nacho pale mtu kafiwa na MAMA/BABA/MTOTO - halafu hata chozi - eti kpaka make-ups - katengeneza hair style ya nguvu - lipstick - golden ear rings etc. halfu macho makavu ..................mh lakini labda mioyo inatofautiana jamani -

halafu kwenye mazishi - kama watu wamekuja kuzika - iwe ni kuzika tu jamani - lakini wengine ni GOSSIPS kwa kwenda mbele - umbeya - kuteta etc.

sijui inakuwaje ...........mie nishawaambia ndugu zangu kwenye mazishi yangu nataka:

1. matarumbeta - nyimbo za kumsifu Mungu kwa sana
2. Watu wote wanastahili kuniwekea maua -sitaki protocol - kwani sina UBAGUZI

3. Mji/Kijiji/Mahali nitakapokufa - nizikwe hapo - sitaki expenses za KUSAFIRI - VYAKULA VYA NJIANI - USUMBUFU TU JAMANI - safari safari hadi mnapinduka njiani .........kha!!

Great Thinkers - Think about this...........................
 
Back
Top Bottom