Ushari: Binti ninaempenda sana kaniibia

Ilikuwa huyo atakuibia mpaka sindano ya kushona. Mkimbie kama ukoma
 
achana na hayo mambo mkuu, afadhali Mungu kakuwekea bayana aina ya msichana unae date nae kabla ya ndoa, mpigie simu na usifiche kitu kwamba ni yeye aliezichukua na kwa hapo ndio mwisho wa mapenzi yenu na hutoweza kuendelea nae na wala huna haja ya kuongea kwa ukali just be gentle. Toa sadaka kwa kumshukuru Mungu kwa kukuweakea wazi aina ya rangi halisi ya huyo dada. Halafu move na life utajisikia amani sana.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,

Kuna binti ni mpenzi wangu tuna miezi 10 sasa toka tunapendana mpaka imefikia kuahidiana kujenga familia moja. Cha kusikitisha na kutia hasira mpaka naomba ushauri kabla sijachukua maamuzi magumu.

Leo kaniambia anakuja kunitembelea. Nikamkubalia na nikamtumia nauli kwani alieleza kuwa hakua na nauli ya kwenda na kurudi.

Baada ya kufika tukapika na kula na stori za hapa na kule pamoja na mambo ya kikubwa. Sasa ilipofika mida fulani tupo geto nikamwagiza mtoto wa jirani dukani kumbe msichana kaona wapi pesa ilikua, baada ya kutoka nje kwenda kumpokea dogo mzigo wangu kumbe msichana kachomoka na mkwanja mrefu na kuficha nyuma ya kava la simu.

Hapo baada ya kumaliza mishe zetu zote nikaamua nimsindikize stendi njiani pindi namkabidhi nauli na mkwanja wake wa kula nikaona minoti ya buku kumikumi nyuma ya simu, nimeshangaa sana japo sijamuuliza japo simu yake nilikua nayo mimi na sikuona pesa yoyote nyuma simu.

Baada ya kurudi geto nikamwambia nimekuta nimeibiwa akashangaa sana kunipa pole. Sasa na mimi nimemwambia hawa majirani watanikoma maana hata begi sijaligusa naenda kwa mganga. Mpaka sasa yupo ananitumia message eti niachane na imani hizo.

Binafsi imeniuma sana na huyu binti nampenda sana lakini kwa hichi nahisi kuchukua uamuzi mgumu kwa sababu sijawahi kumnyima pesa na ninamuhudumia kuliko maelezo.

Ushauri wenu jamani

Nawasilisha
Utakuwa huna hela
 
Back
Top Bottom