Ushari: Binti ninaempenda sana kaniibia

Ushari: Binti ninaempenda sana kaniibia

scientificall

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
460
Reaction score
360
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,

Kuna binti ni mpenzi wangu tuna miezi 10 sasa toka tunapendana mpaka imefikia kuahidiana kujenga familia moja. Cha kusikitisha na kutia hasira mpaka naomba ushauri kabla sijachukua maamuzi magumu.

Leo kaniambia anakuja kunitembelea. Nikamkubalia na nikamtumia nauli kwani alieleza kuwa hakua na nauli ya kwenda na kurudi.

Baada ya kufika tukapika na kula na stori za hapa na kule pamoja na mambo ya kikubwa. Sasa ilipofika mida fulani tupo geto nikamwagiza mtoto wa jirani dukani kumbe msichana kaona wapi pesa ilikua, baada ya kutoka nje kwenda kumpokea dogo mzigo wangu kumbe msichana kachomoka na mkwanja mrefu na kuficha nyuma ya kava la simu.

Hapo baada ya kumaliza mishe zetu zote nikaamua nimsindikize stendi njiani pindi namkabidhi nauli na mkwanja wake wa kula nikaona minoti ya buku kumikumi nyuma ya simu, nimeshangaa sana japo sijamuuliza japo simu yake nilikua nayo mimi na sikuona pesa yoyote nyuma simu.

Baada ya kurudi geto nikamwambia nimekuta nimeibiwa akashangaa sana kunipa pole. Sasa na mimi nimemwambia hawa majirani watanikoma maana hata begi sijaligusa naenda kwa mganga. Mpaka sasa yupo ananitumia message eti niachane na imani hizo.

Binafsi imeniuma sana na huyu binti nampenda sana lakini kwa hichi nahisi kuchukua uamuzi mgumu kwa sababu sijawahi kumnyima pesa na ninamuhudumia kuliko maelezo.

Ushauri wenu jamani

Nawasilisha
 
Mtumie message mwambie unaenda kumsomea Albadiri huyo mtu aliyeiba pesa zako...Lazima Atairudisha hahaha
 
Aiseee. Yaani leo moja yamefanyika yote hayo sio siri mmejua kucheza na muda.

Pia pole sana kwa kuchagua kuwa na kibaka.
 
Mkuu wewe kua mpole, roho itamsuta ataenda dukan atanunua sumu ya panya atakunywa halaf atakufa mkuu.
Ushauri wangu haina haja ya kwenda kwa mganga, labda ukiona kuna ulazima nenda ila usimfanyie kitu kibaya mwambie tu mganga afanye mabadiliko gegedio alihamishie mdomoni na mdomo uhamie kunako gegedio
 
Labda aliona umezidi ubahili, ingekua vyema kuweka kiasi ili tujue tukushauri vipi maana unaweza kuta ele yanyew haifika hata sh elfu 40
 
Aiseee. Yaani leo moja yamefanyika yote hayo sio siri mmejua kucheza na muda.

Pia pole sana kwa kuchagua kuwa na kibaka.
kumbe nawe umeshtukia.. ukiangalia muda hapo unapwaya!
 
Back
Top Bottom