Ushamba wa wamiliki wa vyombo vya moto

Ushamba wa wamiliki wa vyombo vya moto

MGONGA ULIMBO

Member
Joined
Jun 25, 2017
Posts
32
Reaction score
51
NIENDE MOJA KWA MOJA KATIKA MADA HUSIKA.

BINAFSI: Napata shida sana kuwaelewa baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto kama akili zao zipo sawa sawa au ni ushamba au ujinga uliokubuhu.

Kama wewe ni mtembezi mida ya usiku katika jiji la Dar nadhani hata mikoani watakuwepo tu..utaona kuna magari mengi sana yakiwa katika foleni na mwonekano tofauti tofauti wa jinsi taa zao zinavyowaka.Tuende sasa katika kiini cha ushamba wa wamiliki hawa kiasi ambacho kinakera watumiaji wengine wa barabara.

1.Flicker Lights-Sasa hivi umeingia mtindo wakufanya taa za gari zinakuwa zinawakawaka kwa kuzima kama taa za disco.Nawaza hapa sijui Traffic police hawajawai kuligundua hili?.Naamini waliotengeneza magari hawakuwa wajinga kuwa na universal standards kwa magari kama kuwa na taa nyekundu,nyeupe,njano n.k na kila taa zina kazi yake.Nashindwa kuelewa kuwa hawa madereva walipitia vyuo gani..wanashindwa kufahamu dereva anapaswa kuendesha magari matatu..sasa dereva wanyuma atajua vipi kama umefunga break halikuwa taa zako zanyuma zinawakawaka muda wote tu.

2:Led lights-Hizi taa zina mwanga mkali sana muda wote.sasa kuna baadhi ya wamiliki wa pikipiki au magari wanazifunga kwa nyuma.Sijui hawafahamu kuwa zinaumiza macho dereva wanyuma na kufanya asiweze kuona barabara vyema.Pia kuna wengine wameenda mbali zaidi na kuzibadili kuwa ndio kama taa za breki.

3.Ridiculous Lighting-hizi ni mchanganyiko wa taa nyingi katika gari zenye rangi tofauti kiasi ambacho ukiwa barabarani unaweza jua ni Pub inatembea..mpaka utakapokaribia ndipo utajua ni gari.Sasa nawaza huu ujinga wakuweka taa zisizo na maana unatoka wapi,je ni kweli hawana ufahamu kuwa taa hizo huweza kumlaghai dereva mwingine na kumsababishia ajali?

4.One head lamp-hii ni ile gari kutembea na taa moja tu na kumchanganya dereva anayekuja kujua ni pikipiki wakati ni gari..hivi ni kweli hawana pesa ya kununua bulb?

5.Full Lighting-hii ni ile tabia ya madereva hususani wa mabasi ya mkoani kuwasha taa kubwa muda mwingi..sasa sijui ni ujeuri tu ama hawajui kanuni zaidi yakukuimbiza roho za watu.NA NI MABINGWA wa kuovertake..sasa anaovertake unakutana nae kakuwashia full.(fumba macho hapo kinachotokea)

KAMA NA WEWE UNA KERO UNAWEZA KUONGEZEA NDUGU MWANAJAMVI.
 
nikinunua gari nitazifunga na mm ili nione ushamba wake mkuu
 
Back
Top Bottom