UShamba na vioja vyake

CHIBA One

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2018
Posts
558
Reaction score
2,102
Ni kitu gani cha kishamba umewahi kukifanya kwenye maisha yako...?? Baadae uligundua umezingua? (Ushamba ni namna ya kujaribu kufanya kitu kigeni usicho na uelewa nacho)

Binafsi nimewahi kutumwa na dingi nikamtolee pesa ATM nilikuwa natetemeka sana nilipofika na sikufanikiwa badala yake card ilimezwa
 
Ushamba wangu kipindi nina umri wa miaka 10 hivi niliwahi kumeza barafu mjini.

"nilinunua barafu kwa mara ya kwanza siijui sasa nikaiuma kama nusu na kuanza kutafuta, doh hali ya meno ikabadilika ghafla nikahisi kinywa Kizito kama kopo, mbele alikuwepo mgambo nikasema hapa nikitema naweza kukamatwa kwa uchafuzi wa mazingira (Mawazo yalivyokuwa yananituma) nikiangalia pembeni kuna dust bin za keep your city clean. Mwanaume nikameza barafu sitaki ujinga".
 
Darasa la nne siku ya kwanza kuachwa niende home peke yangu nilipitia mnazi mmoja nikazunguka clock tower kutoka shuleni upanga kwenda kupanda daladala posta mpya
 
Mara ya kwanza kupanda ndege (Tz - German via Dubai), seat belt ilinitoa jasho la kengele kuifungua (Sikua na kiwembe tu, kazi ingekua simple). [emoji6]

Mtoto wa kiume nikajikaza roho kumwita Flight Attendant aje anisaidie. Dada alijikaza kiaskari asinicheke, mpaka chozi lili mlenga.[emoji18]
 
Hahahahahaa, salute kwako mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…