Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,780
- 10,710
Wakuu, naomba Leo tuweke ushabiki pembeni tudadavue kama GT uvamizi wa RC pale Clouds TV. Naomba tuangalie mazingira yote kwa uwazi kabisa tuje na conclusive evidence juu ya tukio hilo la kulaaniwa.
1. CCTV FOOTAGE
Anaonekana mkuu wa mkoa akiingia kwenye mlango wa kwanza akifuatiwa na mtu mmoja aliyevaa kiraia hana silaha kisha askari askari mwenye silaha aliyefunga mlango huo. Jumla ya walioingia ni watatu. Halafu anaonekani mkuu wa mkoa akifungua mlango wa pili (wa kuingilia studio?). Anapoanza kuingia ndani footage inakoma
2. USHAHIDI WA MAZINGIRA
Masaa kadhaa baadaye taarifa zinazagaa kwamba clouds wamevamiwa na mkuu wa mkoa akiwa na askari wanane wenye silaha na kuwapiga vibaya sana licha ya kuwatisha watangazaji. Na hapa ndipo shida inapoanzia
...ile footage haithibitishi tykio polite la uvamizi.
*Ukiitazama haioneshi ubabe wowote kwenye kuingia ndani studio. RC aliingia kwa kufungua mlango taratibu
*Nje walikuwapo walinzi ambao hawakushuhudia nia yoyote ya uvamizi mpaka pale walipopigiwa simu na Ruge (aliyekuwa nyumbani kwake). Wao walimwona RC akiingia kawaida tu hapo studio.
*Mazingira ya studio ya tv huwa na camera nyingi tu. Ni ajabu sana kusiwe na kipande japo kifupi cha kile kilichotokea ndani ya studio. Hats hiyo footage, ni kwa nini inakoma pale tu RC anapoanza kuingia ndani? Je, ni kweli kuwa clouds wameweka camera hapo mlangoni tu? Au labda mkuu wa mkoa aliamuru kamera zizimwe kabla ya kuingia ndani?
*Kama kamera zilikuwa mbovu walau tungepata hata audio ya kile kilichitokea ndani basi. Sio masimulizi tu. Hapo ni studio na vifaa vyote vipo. Kwa nini tusadiki masimulizi?
3. RIPOTI YA KAMATI
Kamati ilitoa ripoti kwamba RC alivamia akiwa na askari watano? na si nane. Pia wafanyakazi hawakupigwa kama ilivyoarifiwa hapo awali. Ni kwa nini ilitolewa taarifa kinzani hapo awali?
4. URAFIKI WA RC NA CLOUDS
Ruge anakiri kuwa hawa ni marafiki wa siku nyingi. Tena anatoa kauli tata kuwa RC anatabia ya kwenda hapo studio kupiga stori. Swami hapa, je, kila anapokwenda hutumia utaratibu gani kuingia studio? Je, huwa anaacha wapi walinzi wake? Kuna rekodi yoyote ya clip za cctv za huko nyuma ili tuone ilivyokuwa?
5. Kilichopo mpaka sasa ni ushahidi wa masimulizi ya wanaodaiwa kuvamiwa. Ushahidi wa clip ulikuwa na lengo la kuandaa akili ili wasikilizaji wafanye mwendelezo wa uvamizi akilini mwao. Mtu wa kwanza kabisa kuripoti uvamizi huu alipaswa kuwa mlinzi.
Ni mtazamo wangu tu, baada ya tafakuri ya kina. Twende na constructive criticism kama nilivyofanya mimi, ile timu matusi mkae kando kuruhusu mjadala. Nawasilisha.
Maswali yatokanayo na mjadala unaoendelea :
**kwa nini Gwajima aliripoti kuvamiwa na kupigwa watangazaji? Nani aliyewasiliana naye kumpa habari ili alipue? Was it a coordinated move?
**kwa nini clouds hawataki kuripoti tukio hili polisi? Kwa nini walisubiri liwe magnified na mitandao kwanza? Je, yawezekana walikuwa wanapima upepo? Je kuna yawezekana kuna ofisi ambayo walitarajia itaingilia kati ili kulishughulikia suala hili tofauti na vyombo husika?
**Kwa nini ililazimu waziri kukemea vikali hata kabla ya kujiridhisha usahihi wake? Kwa nini jinai hii haikuhusisha vyombo rasmi vya uchunguzi? Kwa nini haikufanyika coordination na mamlak teuzi ya RC? Kulikuwa na haraka gani ya kukimbilia kwenye press utadhani studio iliteketezwa? What is behind all this!?