YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,995
Sasa hivi boda boda kila kona mijini na vijini tofauti na zamani wanakijiji pia wanapanda boda boda na bajaj na kufanya biashara za bodaboda na bajaji.
Majiji kama Dar es salaam watu wanalalamika foleni kwa kuwa watu wanaomiliki magari binafsi ni wengi mno hadi kusababisha msongamano wa magari hasa asubuhi na jioni.Serikali ya CCM imewasaidia sana kwa kutengeneza mazingira ya kuwawezesha kumiliki hayo magari tofauti na zamani.
Simu za mkononi hata bibi na babu kijijini wanazo tofauti na zamani.Mtu asiyekuwa na simu anaonekana si mshamba bali haeleweki.
Wabunge wote wanauwezo wa kukopa na kumiliki magari ya kifahari tofauti na wakati wa mkoloni ambapo walikuwa hawana uwezo hata wa kukopa baiskeli.
Shule ziko bwerere jichagulie mwanao asome english medium au Swahili medium ni uwezo wako tu Asome za serikali au vyuo binafsi
Sasa hivi hadi akina Godbless lema,Sugu na Msigwa wanaruhusiwa kuwa wabunge kupata posho na kuboresha maisha yao tofauti na zamani .
Saluni na maduka ya vipodozi kila kona kila unayekutana naye kajipodoa kapendeza awe mbunge au la tofauti na zamani ambapo vilikuwa havipo.Siku hizi kwa sababu ya hizo saluni na vipodozi bibi anaonekana baby girl na babu anaonekana baby boy
Anayebeza kazi za serikali ya CCM atakuwa kakolea kiroba.