Ushahidi: Jinsi waliosaidia CCM kwenye uchaguzi mkuu 2015 wanavyoteseka

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,237
Hakuna haja ya porojo, naingia moja kwa moja kwenye vielelezo:

1. Antony Diallo
Huyu ni mtu aliyevunja hata taratibu za TCRA kwa kuhakikisha Star Tv Inaonyesha kampeni za ccm tu , lakini akawa miongoni mwa wahanga wa mwanzo kabisa kusomeshwa namba baada ya StarTV kupigwa kufuli.

2. Nape Nnauye
Kwa mujibu wa kauli yake mwenyewe ni kwamba Alitumia nusu ya uhai wake kulala porini ili kunusuru ccm , lakini malipo yake ni kutishiwa Bastola na mtu asiyejulikana ambaye hakuwahi kulala porini hata mara moja.

3. Yusuph Manji
Huyu alitumia utajiri wake kuhakikisha CCM inashinda kata ya Kijichi na Mbagala Kuu ikiwa ni pamoja na jimbo jipya la Mbagala, Malipo yake ni kuwekwa selo kwa tuhuma zilizokosa uthibitisho.

4. Monaban
Wanaomfahamu wanadai hata zile kura kidogo ilizopata CCM jimbo la Arusha zilitokana na umaarufu wake na imani ya wananchi kwake, malipo yake ni kunyang'anywa kiwanda cha unga.

5. Wema Sepetu
Hakuna asiyefahamu misele aliyoifanya huyu dada katika kurubuni wananchi ili waichague CCM, huku akijua kwamba haitaweza kuleta maendeleo, maana ilishashindwa kwa karibu miaka 60, Malipo yake ni kuhusishwa na Uuzaji na ulaji wa unga pamoja na Bangi (kesi ingali inaunguruma mahakamani )

6. Diamond Platnamz
Huyu ni miongoni mwa wanamuziki wa Kitanzania wenye washabiki lukuki na hasa vijana. Taarifa zinaonyesha kwamba umati wa vijana wengi kwenye mikutano ya CCM ulimfuata yeye, na ndio maana hata kwenye utumbuizaji alikuwa akiwekwa mwisho. Malipo ya kazi yake mmeyaona, nyimbo zake zimepigwa pini na kuna tetesi kwamba atakamatwa muda wowote, sababu zinajulikana.

7. Erick Shigongo
Inasemekana huyu ndio aliyechukua tenda ya kutengeneza fulana na kofia zote za kiwango cha chini zilizotumika kuwanunua wananchi wa vijijini. Alishaonekana kwenye vyombo vya habari akimwaga chozi kwa kudhulumiwa malipo yake.

8. Shitambala
Huyu mtu alivuma kwa usaliti wake kwa chma chake cha zamani CHADEMA , kwa wakati ule haikuwa rahisi kuuza ubunge mchana kweupe, lakini yeye aliweza na akatunukiwa uenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya, alishiriki katika kampeni ya kumg'oa RAIS WA MBEYA bila mafanikio na akaangukia pua iliyoambatana na fuvu la kichwa .

Huyu ni Wakili wa kujitegemea na kwa hali ya mambo ilipofikia HAJAPATA KUSIMAMIA HATA KESI YA KUKU KWA MWAKA WA PILI SASA.

9. Evarist Chahali
Taarifa zinadokeza kwamba huyu ni miongoni mwa "Watu wasiojulikana A.K.A Kitengo". Juhudi zake za kuipigania CCM kupitia maandishi kadhaa zinafahamika, LAKINI ALICHOAMBULIA NI MAISHA YA DIGIDIGI .

10. Mwigulu Nchemba
Harakati za gizani alizotenda mtu huyu ikiwemo kutengeneza filamu ya ugaidi wa Lwakatare, lugha za kejeli kuhusiana na viroba vyenye miili ya binadamu vilivyookotwa kwenye bahari ya hindi, kupotea kwa Ben Saa nane na wengine, usingedhani kama angeweza kudhalilishwa kiasi hiki.

11. Peter Zakaria ( Tajiri wa Tarime )
Huyu ushahidi wa vielelezo visivyo na chembe ya shaka unaonyesha kwamba Mabasi yake yalitumika kusomba wananchi mbalimbali wilayani Tarime na kwingineko ili kujaza mikutano ya kampeni ya ccm , mapicha ya mgombea urais wa ccm yalijazwa hata kwenye side mirror kiasi cha kuvunja hata sheria za usalama wa barabara , lakini amenusurika kutekwa na sasa anapambana na hali yake , ni miongoni mwa wanunua shahada maarufu huko Tarime kwa manufaa ya ccm

12. Yusufu Makamba

............

13. Abdulrahman Kinana
.............

14. January Makamba
................

15. William Ngeleja
....................

16.
.......................

Zingatia - Majina yataendelea kuboreshwa kwa kadiri ya tutakavyoyakumbuka.

Lakini je mambo haya yanatokea kwa bahati mbaya ? La hasha ! Maana maandiko matakatifu yanasema hivi " KILA ATENDAYE DHAMBI ATAHUKUMIWA "

Naomba kuwasilisha .
 
Kila atendaye dhambi atahukumiwa kwa kadri ya matendoyake naongeza.
Watu wasiojulikana watajulikana tu hata malaika mkuu akianza kuongoza malaika wadogo.

Ukifanya vizuri hapa dunianaini unafanya kwa ajili yako wewe mwenyewe.
Na ukifanya matendo mabaya pia unajifanyia wewe mwenyewe.
Mwisho wa mabaya ni mauti.
 
diamond pia usimsahau mkuu maana bila yy nazani ata uwanja usingejaa ila sahivi ata support ya waziri wake hakuna
 
Hata waliopigania chadema kwa jasho na damu kwa sasa wanataabika,wamekufa , na wengine wanajiengua kila kukicha,anaefaidi ruzuku ni Mbowe na familia take,ndio dunia ilivyo,nyani haoni kundule
Mbaya zaidi Ccm tumekula Ruzuku haijatosha tumeanza kula na nyama za Binadamu.
Risasi mchana kweupe,
Viroba na Sandarusi si vina tuhusu sisi?
Alafu hatujatosheka bado tunataka tuwe Malaika mkuu.
 
Mbaya zaidi Ccm tumekula Ruzuku haijatosha tumeanza kula na nyama za Binadamu.
Risasi mchana kweupe,
Viroba na Sandarusi si vina tuhusu sisi?
Alafu hatujatosheka bado tunataka tuwe Malaika mkuu.
Vipi chacha wangwe na yule diwani dar wapo hai?
 
8. Lemutuz
Kipindi cha kampeni alitumika sana kwenye mitandao.
Nakuhangaika kote kuita Le field Marshall le kamanda magufuli. Lakini ndo kwanza hatahapewi teuzi yoyote ata kuwa secretary wa UMOJA WA WANAWAKE CCM bado wamemnyima.

Mange ameshusha video zake za uchi hakuna CCM aliemtetea kweli CCM ni wakatili wanamuonea huyu mzee asie kua.
 
Back
Top Bottom