Ushabiki wa Simba-Yanga wavuruga ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushabiki wa Simba-Yanga wavuruga ndoa

Discussion in 'Sports' started by M-bongotz, Mar 10, 2010.

 1. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  USHINDI wa mabao 3-1 ilioupata Simba dhidi ya JKT Ruvu, Jumamosi ulisababisha kizazaa kwenye maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam kati ya wanandoa.

  Wanandoa hao ambao mwanaume ni shabiki wa Yanga na mkewe shabiki wa Simba walijikuta hawaelewani.

  Mwandishi wa Mwananchi alishuhudia tukio baina ya wanandoa hao wakigombea redio baada ya Simba kushinda.

  Wanandoa hao wakisikiliza redio huku ubishi baina yao ukiendelea, uligeuka baada ya Simba kufunga bao la kwanza na ndipo mwanaume ambaye ni shabiki wa Yanga alipoikimbilia redio na kuizima.

  Mwanaume huyo ( jina tunalo) alipozima redio hiyo ndipo ugomvi mkubwa uliibuka baada ya mwanamke(jina pia tunalo) akidai mumewe aiwashe redio asikilize jinsi timu yake anayoipenda ilivyokuwa ikicheza.

  Mwanaume huyo alikataa na kumweleza mkewe, "Nende ndani ukalale, mwanamke gani unayependa kushabikia mpira kama wanaume, ondoka hapa, la sivyo nitakupiga".

  Mwanamke huyo alipoona mumewe huyo kapandwa na jazba na kuzima redio alimwambia," Leo hii ukinipiga na mimi sikupi unyumba tuone nani zaidi."

  Kitendo kile kilimudhi mume wake ambaye alianza kumshushia kipigo mkewe huku akimtamkia kuwa atampa talaka.

  Hadi Mwananchi inaondoka katika tukio hilo, ugomvi mkubwa uliotokana na ushabiki wa Simba, Yanga ulikuwa ukiendelea na kuvuta watu wengi wakiwa na shauku ya kujua kilichokuwa kikitokea.


  Source: Mwananchi
   
Loading...