Ushabiki wa mpira

Curious Naturally

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
528
Reaction score
523
Wandugu, mimi kwa sasa hivi sio mshabiki wa timu yoyote ya mpira, ila ninapenda sana ninavyoona watu wanaongelea mpira. Najisikia aibu pale ninapoulizwa kuhusu mpira wa majuu, coz siufuatilii.
Kwa mwaka huu nimehamasika, so naomba mnijuze yafuatayo..

1.Nianzeje ili angalau niweze kuujua mpira vizuri
2. Nishabikie timu gani Nyumbani na ulaya?
 
Kwa hapa nyumbani chama la ukweli ambalo ukishabikia hupati stress basi shabikia timu ya wananchi DAR YOUNG AFRICANS(yanga),
Ulaya shabikia MANCHESTER UNITED.
 
Kwa hapa nyumbani chama la ukweli ambalo ukishabikia hupati stress basi shabikia timu ya wananchi DAR YOUNG AFRICANS(yanga),
Ulaya shabikia MANCHESTER UNITED.



timu hata uwanja haina!! mkifungwa kwenye bonanza mnafukuza kocha!!



Timu ya kushabikia kwa watu wenye akili ni Azam fc tu!!

kwa ulaya tupo pamoja
 

Anzia kwenye ndondo kijijini kwenu. Siku ukiwa tayari hutauliza maswali haya
 
Duuu tangu lini mtu akaushauriwa timu ya kushabikia? Makubwa mi najua mtu ukiwa unakuwa unaanza ushabiki baadae "automatically" ukajikuta shabiki wa timu fulani lakini si kwa kushauriwa, kama ni hivyo mm nakushauri kwa bongo shabikia Ndanda fc na ulaya shabikia QPR ndio timu za hadhi yako
Baadae ukishaona uchungu wa kufungwa ndio uje tena hapa jukwaan tutakupandisha daraja kwa kushabikia timu kubwa kubwa, lakini kwa sasa tukikupa timu kubwa itakuwa tumeku"overdose" mkuu
 
timu hata uwanja haina!! mkifungwa kwenye bonanza mnafukuza kocha!!



Timu ya kushabikia kwa watu wenye akili ni Azam fc tu!!

kwa ulaya tupo pamoja

Hata isiwe na uwanja ilimradi tu mimi inanipa raha, hiyo ndo yanga bhana tunapiga nne nne huko Zenj. Ninyi wenye uwanja full stress kila kukicha na Omog wenu.
 

Ili Uanze Kuujua Mpira Vizuri Kwanza Anza Kujifunza Kuwa Mbishi Tena Wa Kukaribia Kupigana au Kupigwa Kisha Jifunze Sana Matusi Ya Kiswahili Na Ya Kizungu Na Uyakariri Vilivyo Na Uwe Tayari Kuyatumia Either Kwa Kumsifia Mchazaji Or Kwa Kumponda Mchezaji. Kuhusu Ushabikie Timu Gani Hapa Nyumbani Nakuomba Sana Na Chonde Chonde Shabikia Timu Ya Mwenyezi Mungu Pamoja Na Malaika Wake Mkuu GENTAMYCINE Ya Simba Sports Club Na Ole Wako Ushabikie Matahaira Yanga Kwani Hautakuwa Na Muda Mrefu Wa Kuishi Hapa Duniani Kutokana Na Stress Utakayoipata Huko Haswa Kwa Kufungwa Na Mnyama Simba Kila Ukutanapo Nasi. Kwa Ulaya Wala Usipate Taabu Shabikia Timu Ya Liverpool FC Kwani You Will Never Walk Alone Na Kwa Timu Za Taifa Wewe Wala USIPOTEZE MUDA Wako Shabikia Tu Timu Ya Taifa Stars Hii Ya MABORESHO. Nadhani Nimekusaidia, Kila La Kheri.
 

Noted! nashukuru sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…