Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,826
- 730,265
Hii ni aina ya uchawi ambao husambazwa kwa kupulizwa uko kwenye mfumo wa unga unga (sio madawa ya kulevya)
Usembe ni mbaya usembe hapigwi mtu mmoja bali kikundi cha watu maranyingi kitongoji kizima ama kijiji..mkipuliziwa usembe mtajikuta wote mnakuwa kama akili zimepooza..mnakuwa hamko katika maamuzi yenu binafsi mtatenda mtakachoamrishwa au kuambiwa
katika ishu nzima ya kutoa wachawi kwenye miji na vijiji usembe hutumika kwenye zile sehemu ambazo watu ni wakaidi wa kutaja wachawi wao ama kukataa kutoa ushitikiano kwa mganga
Basi nimenikuta tu asubuhi hii natabasamu nilipokumbuka ya usembe na sembe na muvi nzima ya wiki hii kuhusiana na madawa ya kulevya