Usawa kwenye siasa ni muhimu

Usawa kwenye siasa ni muhimu

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
409
Reaction score
343
Wanabodi,

Walio wengi wameridhika na uongozi wa Rais Samia katika muda mfupi ambao amekuwepo madarakani. Ila kitu ambacho ni kawaida kwa kiongozi yoyote ni minong'ono ya hapa na pale kutoka kwa kundi la watu ambao sio wengi lakini hawa kubaliani na maamuzi au mienendo ya serikali.

Wengi wamekuwa waki lalamika sana kuhusu nguvu inayotumiwa na vyombo vya usalama kudidimiza demokrasia na kuminya haki, Tofauti na hayo yote tunayo fahamu, kuna kitu kipi kingine kinacho onyesha kwamba bado hatujawa na demokrasia ya kweli?.

Kwanza kabisa, kabla ya kuishutumu serikali kuhusu hali ya kisiasa iliyopo sasa hivi, tuangalie wawakilishi wa wananchi bungeni. Utagundua kwamba baada ya uchaguzi uliofanyika mwaka 2020, wawakilishi kutoka vyama vya upinzani walikuwa 8 tu. Ndiyo, wabunge 256 wa CCM walipigiwa kura na watanzania walio wengi lakini ili kuwa na majadiliano yenye manufaa zaidi na mawazo yaliyofikiriwa kwa kina zaidi, ni muhimu kuwa na upinzani.

Maoni tofauti haimaanishi kuikosoa serikali tu bali kuhakikisha kwamba wananchi wana nufaika na uongozi. Sio sahihi kwa mswada wowote kupita bungeni kwa asilimia 100, sio sahihi kwa Mhe Tulia Ackson kushinda uchaguzi wa uspika kwa asilimia 100. Chama cha mapinduzi kuwa na asilimia 100 ya wabunge ni dalili kubwa sana ya udikteta.

Mungo ni mwema, wakati wote
 
Back
Top Bottom