Usawa kwenye Mapenzi, Ubaguzi kwenye Infidelity.

Usawa kwenye Mapenzi, Ubaguzi kwenye Infidelity.

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,507
Neno WAPENZI katika mahusiano linakuwa na maana nyingi kutokana na mazingira na aina ya PENZI linalokuwepo katika wapenzi. Penzi linajengwa kwa UAMINIFU kati ya wapenzi.

Historia imebainisha katika jamii kuwepo kwa matendo ambayo yanaondoa uaminifu katika penzi kitu ambacho kinasabisha wapenzi kutokuwa na penzi tena na matokeo yake ni kuamua kuanza kulijenga penzi tena au kila mmoja kuanza kulitafuta penzi sehemu nyingine.

Hii inanipeleka kwenye usawa wa penzi ambapo historia imebainisha pale mwanamme anapobainika kuwa yeye ndiye kichocheo cha kutokuwepo uaminifu katika penzi (cheater) mara nyingi wanawake huwa wanasamehe na kuanza kulijenga penzi tena lakini pale kitendo kama hicho kinapotokea kuwa mwanamke akawa ndiyo kichocheo, mwanamme ni mara chache sana kusamehe na kuanza kulijenga penzi tena.

Kwa kifupi, kwa nini ninyi wanawake mnapenda mara nyingi kuwasamehe wanamme wenu ambao ni wazinifu (cheater) lakini wanamme wenu hawapendi kuwasamehe ninyi pindi mnapofanya pia tendo kama hilo?.

Kwa nini wanamme tunapenda kusamehewa tunapo cheat, stray or lies lakini sisi mara nyingi hatupendi kuwasamehe wanawake wetu wanapofanya pia mambo kama hayo?.

Kwa nini pawepo usawa katika penzi na ubaguzi katika kuzini (infidelity).
 
Back
Top Bottom