Usanii wa Waingereza sasa wanagoma kuondoka EU!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Baada ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Umoja wa Ulaya (EU) , Umoja huo umeitaka nchi ya Uingereza kuharakisha mambo na kuondoka mara moja yaani kujivua uanachama na kutengana nao, lkn nchi hiyo inayojulikana kwa sifa kubwa ya unafiki, Uingereza ikiongozwa na pro Brexit (Boris Johnson) mkubwa ambaye anawania Uwaziri Mkuu wa nchi hiyo wamegoma kuondoka EU haraka iwezekanavyo kama EU inavyowataka, matokeo yake wanataka kujadiliana na EU ili wabakize privileges yaani kwa kifupi hawataki kuwa wanachama wa EU lkn wanataka faida zote za kuwa Mwanachama wa EU kama vile wanataka wabakie kwenye soko la pamoja la EU, wanataka raia wa Uingereza waendelee kuwa na haki zote kwenye nchi nyingine za EU kama kufanya kazi bila ya vibali vya kazi, kusoma n.k lkn wkt huwo huwo wakiwa siyo Wanachama wa Umoja huwo!

Huwo ndiyo unafiki wa Waingereza, kelele nyingi lkn kumbe ni ubinafsi tu ndiyo unawasukuma, sasa Kiongozi wa nchi hiyo ambaye ametangaza kujiuzulu hapo Oktoba mwaka huu amekataa kuanza mchato wa kujitoa na kujitenga umoja huo ambapo EU walitaka ufanyike mara moja ili waweze kuendelea na mambo mengine!
 
Waingereza wapo special hata hivyo.


Hawana uspecial wowote ni wanafiki tu, kama wangekuwa special wangeondoka mara moja EU, kuna nchi special Ulaya ambazo zimejitosheleza kama vile Norway, Uswisi hao ndiyo hawana shida na EU lkn Uingereza hawezi kuishi bila EU kinachowasukuma ni unafiki, sasa Scotland wanataka kuwa sehemu ya EU ina maana watajitenga na UK !
 
Back
Top Bottom