Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,374
- 72,891
Mtu yeyote mwenye kuangalia kwa jicho la tatu suala la Mkurugenzi wa jiji la Dar Bw. Wilson Kabwe kusimamishwa kazi ataiona hadaa kubwa iliyopo nyuma ya maamuzi hayo inayofanywa na CCM.
Bw.Kabwe kwa zaidi ya miaka 10 amepigiwa kelele juu ya matendo yake akiwa Mkurugenzi Mwanza na Mbeya mpaka ndani ya Bunge lakini kwa vile humo kote alikuwa anafanikisha malengo ya Chama alilindwa dhahiri na chama pamoja na PM mstaafu Pinda na hakuna hatua iliyo chukuliwa.
Ni wazi kuwa baada ya jiji LA Dar halmashauri zake kuangukia mikononi mwa Upinzani na Stand ya Ubungo, Parking fee, Machinga complex kuwa ni moja ya ajenda zao ili kuokoa mapato ya jiji umepangwa mkakati wa haraka kuficha aibu hiyo ili ionekane serikali kuu ya ccm imechukua hata dhidi ya Kabwe.
Siku zote kelele hizo dhidi ya huyu bwana walikuwa hawasikii? Vipi na zile kelele za Mwanza kuhusu mradi wa Clinic? Na viwanja vya Luchelele?
Fedha za fidia za NSSF? Bila kuwashughulikia na waliokuwa wanamlinda hiyo itakuwa ni kafara tuu kuficha aibu ambayo ingebumbuliwa na Halnashauri ya Ukawa.
Hata kusimama kwa Makonda na kusema yale kisha Rais kunsimamisha kazi sio suala LA bahati mbaya ila ni jambo lililokuwa limepangwa kuongeza kukubalika lakini wajuaji wametambua.
Mhe. Magufuli endelea kuchukua hatua, lakini usingoje mpaka pale ambapo unabidi ufanye kwa ajili ya kulinda heshima ya CCM