Mkuu kima cha chini wamepunguziwa hiyo asilimia moja ongezeko la mshahara wao sasa unaongezeko la Tshs 62,320/= je mkuu hilo si ongezeko?
Tupe hiyo calculation, usimeze maneno ya mafisadi kama yalivyo. Lazima uufahamu ugeugeu wa mafisadi kwanza kabla ya kuamini kile wanachokisema. BTW Kikwete aliposema kwamba mishahara ya watumishi itapanda, hakusema kwamba ni kwa kima cha chini tu--alisema mishahara ingepanda kwa watumishi wote. Hebu ona kauli zao zinavyogongana hapa:
Msikilize Kikwete
Mishahara ya watumishi itapanda na PAYE itapunguzwa hadi tarakimu moja (1-9)
Rais Jakaya Kikwete ametoa ahadi mbili za kuwafurahisha wafanyakazi. Kwanza ametangaza nia ya kuongeza mishahara yao na pili, kupunguza kodi inayokatwa kwenye mishahara hiyo mambo ambayo ameahidi kutekelezwa katika Bajeti ya mwaka 2014/2015 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema anatambua kuwa wafanyakazi wana hamu ya kujua Serikali itasema nini kuhusu masilahi yao.
Alisema malalamiko ya wafanyakazi wengi ni kutaka kuona kima cha chini cha mshahara kinaongezwa huku kodi kwenye mishahara (Paye), ikipungua.
Mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kufanya hivyo, tumethibitisha miaka iliyopita na tutaendelea kuwa hivyo, alisema.
Huku akishangiliwa na wafanyakazi waliofurika katika Uwanja wa Uhuru, Rais Kikwete alisema: Najua kuwa nyongeza tuliyotoa mwaka jana si kubwa kama wafanyakazi walivyotaka iwe
hata mimi nisingependa iwe hivyo.
Kwa nyongeza iliyofanywa mwaka jana, hivi sasa Serikali inatumia asilimia 44.9 ya Bajeti kulipa mishahara ambayo ni asilimia 10 ya Pato la Taifa.
Akifafanua namna Serikali ilivyofikia uamuzi wa kuongeza mishahara kwa mwaka huu, Rais Kikwete alisema kulikuwa na mjadala mkali baina ya wafadhili waliodai nyongeza ni kubwa mno.
Ni kweli mapato yetu ni madogo lakini kwa kuwa mishahara ni midogo, lazima tuendelee kuongeza, hata hicho kidogo lazima ukitoe ili uijenge ile nafuu, alisema bila kutaja kiwango kitakachoongozwa.
Hata sasa kumekuwa na ubishi mkali kati ya Wizara ya Utumishi na Hazina kuhusu nyongeza ya mwaka huu iwe mpaka kiasi gani, nikaingilia kati nikakubaliana na utumishi, Hazina walikuwa wanataka ipingue kidogo, alisema.
Chanzo: Mwananchi.
Msikikize waziri wa Kikwete:
PAYE kushuka kufikia dijiti moja 2018- Serikali
Serikali imesema Kodi ya Lipa Kadri Unavyopata (PAYE) itaendelea kushuka taratibu hadi mwaka 2018 ndipo itafikia dijiti moja.
Akitolea ufafanuzi wa hoja zilizotolewa na wabunge wengi bungeni jana wakati wa kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2014, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi, Celina Kombani, alisema uamuzi huo ni majadiliano ya pamoja na vyama vya wafanyakazi.
Alisema kabla ya kutoa uamuzi huo walikaa na vyama vya wafanyakazi na kukubaliana iwe inashuka kwa asilimia moja kila mwaka na kwamba hadi itakafofika 2018 ndipo itakuwa asilimia tisa inayopigiwa kelele na wabunge.
Huo si uamuzi wetu, wenyewe tumekubaliana na vyama vya wafanyakazi hivyo ifikapo 2018, ndipo PAYE itafikia single digit ya asilimia tisa, alisema Kombani.
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, alisema lengo la kodi kutoshuka kwa kiasi hicho kwa sasa ni kutokana na majukumu mengi ambayo serikali inakabiliwa nayo kwa wakati huu ambayo yote yanahitaji fedha.
Alisema inakabiliwa na uchaguzi mkuu, uchaguzi wa serikali za mitaa, daftari la wapiga kura na kwamba yote hayo yanahitaji fedha wakati vyanzo vya mapato vikiwa ni vile vile.
MUSWADA WAPITA
Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2014 umepitishwa bungeni jana baada ya kuanza kujadiliwa tangu juzi jioni huku idadi kubwa ya wabunge wakiendelea kulalamikia ongezeko la kodi ya magari yaliyotumika pamoja na PAYE.
Suala lingine lililozua mjadala mkubwa ni kitendo cha serikali kuzembea katika kudhibiti zao la ngozi ambalo wabunge wengi wamedai zimekuwa zikitoroshwa nje kinyemela na kuinyima serikali mapato.
Wakichangia muswada huo baadhi ya wabunge walisema kitendo cha serikali kupunguza kodi ya magari mapya kuendelea kuwa juu huku ya magari chakavu ikizidi kupanda ni kitanzi kwa Watanzania kushindwa kumudu kununua magari.
Mbunge wa Ubungo, Jonh Mnyika (Chadema), akichangia muswada huo alisema kila Mtanzania anapenda kumiliki gari jipya lakini kutokana na kodi na kuwa juu ndiyo maana hununua magari yaliyotumika.
Hammad Rashid (Wawi-CUF), alisema tatizo kubwa ni kufa kwa viwanda vya ngozi Tanzania wakati vile vya Kenya vikiendelea kufanya kazi, hivyo serikali haina budi kuimarisha viwanda vya ngozi nchini.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI