tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 25,990
- 25,384
Usanii wa serikali sikivu ya CCM kwa watanzania ndio utakaochangia kwa kiasi kikubwa kuing'oa madarakani mwaka 2015. Kila mtu ni shahidi jinsi serikali hii inavyowadhihaki watanzania ktk mambo muhimu yanayohusu maisha na ustawi wao.
Katika sherehe za mei mosi mwaka huu, Mh Dr Jakaya Mrisho Kikwete aliahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi na kupunguza kodi ya mishahara (PAYE) hadi tarakimu 1. Kilichotekelezwa ktk bajeti hii ya serikali, kila mtu anakijua.
Ni dhahiri kwamba serikali ya CCM imefikia hatua mbaya ya kuwadhihaki na kuwadharau wafanyakazi, pamoja na mchango wao mkubwa ktk maendeleo ya nchi hii. Mtakumbuka mwaka jana rais JK aliitisha mkutano na makada wa CCM, aliowabatiza jina la 'Wazee wa Dar es Salaam', ambapo alitumia mkutano huo kuwananga wafanyakazi kwa kutamka hadharani kwamba HAHITAJI KURA ZAO!
Naomba nimkumbushe JK kuwa ni wafanyakazi hao hao WENYE NJAA ndio watakaoiangusha CCM yake mwaka 2015. Uzezeta wa wafanyakazi (hasa walimu) sasa basi--ni wakati wa JINO kwa JINO!
Nawasilisha.