Habari wana Jf
Napenda kuuliza mwenye kuimanya vizuri hii kampuni ya Usangu Logistics maana nilipata mashaka makubwa sana mbunge mmoja aliposimama kusema kuwa kampuni hii ilipewa tenda ya kusambaza transforma 10 hapa hapa Dar es Salaam kwa gharama ya Mill. 240 huku kampuni nyingine iliyokuwa imeshindanishwa nayo ikiachwa wakati walikuwa na gharama ndogo zaidi ya sh. Mill. 10 tu.
Mambo haya yaliibuliwa wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya wizara ya nishati na madini, ajabu ile hoja ilizimika tu kiulaini.
Nashawishika kuimanya hii kampuni ni ya akina nani then kutoka hapo tunaconnect the dots.
Nawasilisha.
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
usangu,plantinum credit,smart oil,jembe ni jembe,kilimanjaro pub,cosmopolitan hotel na musa transporter yote mali ya salva rweyamamu wa ikulu
Chizi Fureshi kutokana na kwamba ile siku ilikuwa inawasilishwa bajeti ya wizara ya nishati na madini basi tunafikia conclusion kuwa zile ni transforma hizi za tanesco zilikuwa zinazungumziwa na sio hizi za redio. Tumuombe Tyta kwa hisani ya #TeamWekaPicha atuwekee picha ya hizo ndude.Ndugu yangu deonova hebu jaribu kuja hapa kama GT. Sema sasa hizo transformer(s) ni za kwenye redio au hizi za tanesco na ni model gani. Karibu mkuu.
huyo mwenye kusafirisha transforma 10 kwa 10M labda alidhan ni kusambaza maembe
kumbuk transforma moja ni 5Tonnes
Jana nimeona gari ndogo waliyochangia kwenye taasisi ya dini....gari hiyo ilianeikwa
" SOMA QURAN"
"DONATED BY USANGU LOGISTICS"
Wa TZ acheni majungu na roho ya wivu, kamwe hamuwezi kupiga hatua za maendeleo kama tabia hiyo hamto wachana nayo!