Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,429
USAMBAZAJI WA UMEME MUSOMA VIJIJINI
Jimbo letu lina Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374
(i) Umeme ndani ya Vijiji 68:
Vijiji vyote 68 vimewekewa miundombinu ya usambazaji wa umeme
Kazi iliyokamilishwa Vijijini: 100%
(ii) Umeme ndani ya Vitongoji 374
(a) Mwaka wa Fedha 2024/25:
Wakandarasi 2 wako kazini kusambaza umeme kwenye Vitongoji 74. Kazi itakamilika Disemba 2025
Kazi hiyo ikikamilika Disemba 2025, Jimbo letu litakuwa limebakiza Vitongoji 100 kati ya 374
Kazi itakayokuwa imekamilishwa Dec 2025:
Vitongoji 274 kati ya 374: 73.26%
(b) Mwaka wa Fedha 2025/26
Vitongoji ndani ya Bajeti: 50 kati ya 100 vilivyosalia
Kazi ya usambazaji inaanza 1.7.2025
SHUKRANI
Wananchi na Viongozi wao wa ngazi mbalimbali wa Jimbo la Musoma Vijijini wanatoa shukrani nyingi kwa Serikali yetu inayoongozwa vizuri na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo na ustawi wa Jimbo letu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumamosi, 10 April 2025