Usaliti wa bara la Afrika na dhana ya ukombozi

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,807
Hakuna mbari yoyote ya wanadamu katika historia ya dunia, mbari ya watu walioteswa, walioonewa na kufanyiwa maangamizi ya ajabu kama mbari ya watu wa afrika.

Africa imepitishwa katika misiba na masahibu ya kutisha sana ya wa biashara ya utumwa iliyoanzishwa kidodo kidogo miaka ya 1200 mwishoni, na kushika kasi sana. Na kuanza kufifia si kwa kuwa walioianzisha walikuwa na huruma sana, bali viwanda vilianza kugunduliwa mwanzoni mwa karne ya 1800 na mwafrika kwa mara nyingine tena akaonekana hana faida.

Niani chkula kikiisha melini, au wakiumwa, u kukiwa na tufani basi mzigo wa kwanza kutoswa baharini ulikuwa ni mwafrika. Huku utumwani waafrika walidhalilishwa, hata katika sensa walihesabiwa kama nusu watu, waliuswa kama mifugo mingine na pia kuzalishwa kwa mtindo wa kubreed wanyama.

Waliobaki nyuma wakaishi misituni kama wanyama kwa miaka 600 wakiwa na hofu, utajengaje huku unawindwa kama swala, utashonaje, utaruhusuje mwanao aondoke mbele za macho yako aende "shule" na huku naye anawindwa. Mtafumaje nguo na kuzivaa? Mtauzianaje bidhaa! Ndio sababu ya uduni uliokuwepo kabla ya upepo wa uhuru (wind of change) wa miaka ya 1960.

Baada ya miaka 600 ya utumwa, kukawa na kipindi kingine cha miaka 100 na zaidi ya ukoloni wa mateso sana. Na kisha hata katika uhuru kukawa na ukoloni mambo leo wa kutuambia cha kufanya na kutuhujumu na kutufarakanisha. Kipindi cha vita baridi.

Vita baridi london lakini angola haikuwa ilikuwa ni mito ya damu na machozi. Vita baridi washington lakini kongo kinshasa na katanga ilikuwa ni matanga. Vita baridi, moscow lakini msumbiji ilikuwa ni jinamizi.

Nisiseme mengi sikiliza video ila mateso haya yaliwezeshwa na usaliti wa mwafrika mwenyewe.


 
Back
Top Bottom