Ingawa bado tafsiri ya mapenzi inatafsiriwa kwa upana mkubwa lakini bado pia maana ya mapenzi imesahaulika hali inayofanya mapenzi ya siku hizi kuwa ya kudanganyana na uongo huo wengi wanaupenda.
Usaliti ktk mapenzi ni hadithi ndefu yenye mikasa na visa vinavyoumizwa hasa kwa wale walopata gonjwa hilo.Usaliti mara zote humfanya mtu kuwa katili katika mapenzi na kupelekea matukio mengi na mikasa mingi ktk mapenzi na mwisho wa siku ni majuto kwa wapendanao.
Pepo la usaliti linapoingia ktk mahusiano ya wapendano huwa chanzo cha ukatili na wakati mwingine hata utu kupotea.Yote hayo ni kufanya usaliti kwa mpenzi wako.Usaliti mdogo utazua majuto makubwa.