Usalama wetu ni zaidi ya kanuni

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Suala la kutekwa kwa wananchi si suala nyeti kwa bunge letu. Wapi kama taifa tunaipeleka nchi yetu,hivi kutekwa kwa raia wenye dhamana na nchi yao si nyeti lakini faru john kufa kwake gharama zinatumika kujua chanzo cha kifo.

Umuhimu wa taifa lolote duniani ni wananchi wake,ikiwa taifa linathamini wanyama na kuupuza wananchi wake hapo kuna taifa kweli,mnyama anaundiwa tume,haki ya raia ya kikatiba ya kuishi inatishiwa kiongozi wa bunge haoni umuhimu wa haki hiyo ya msingi ilihali chombo hicho ndicho chenye kutunga sheria lakini kinathubutu kuikanyaga katiba hiyo hiyo.

Lini tutakuwa wazalendo kwa taifa na wananchi wetu ikiwa hata vyombo vyetu vya uwakilishi vinatugeuka. Dr. Tulia wewe ni binti unategemea kuwa mama,hekima na busara katika kutimiza majukumu yako vitaleta tija na heshima kwa chombo unachokiongoza kuliko kufikiria kutengeneza sifa kwa watawala.

Kanuni zako hazioni umuhimu wa usalama wa wananchi,wananchi wanapotezwa,wabunge na mawaziri wanatishiwa usalama wao na serikali yao kwa mujibu wa maelezo ya mh. Bashe,lakini badala ya bunge kustuka na kuzifanyia kazi taarifa hizo,bunge linazipinga,mnataka wananchi tukimbilie wapi?
 
Back
Top Bottom