Jc Simba
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 300
- 423
Habari za asubuhi wote kwa pamoja ?
Natumai wote ni wazima Wa afya, kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza .
Ni kwamba kwa sasa usalama Wa RAIA na Mali zao umekua Wa mashaka makubwa katika Nchi yetu . Kubwa la kutiliwa mashaka ni kwamba hata wenye mamlaka husika wameonyesha kuzidiwa na kuwa kimnya au kukosa majibu pale wanapohitajika kuyatoa majibu hayo .
Watu kutekwa ni jibu moja kwamba kuna shida sehemu ila sasa watu wanatekwa pamoja na Mali kama Roma alivyotekwa yeye pamoja na wenzake na baadhi ya Mali zake kama laptop na CCTV system .
Ukiangalia kilichotokea mpaka watekaji kuamua kuchukua CCTV system ni kwamba wanataka ushahidi usiwepo yaani kuficha ukweli . CCTV system ina tabia ya kuumbua watu sasa wao wakaona ni bora waondoe ili isijewekwa video hadharani na kuwaonyesha.
Lakini hili linakua Kubwa zaidi pale wabunge nao wanapolalala tena Wa chama tawala ili hali tulifikiri ni wakosoaji tu ndio wanaotekwa kwa kipaza sauti za kuikosoa serikali yao pale inapoleta shida au kufanya tofauti na matakwa ya wananchi wake.
Katika sitofahamu ya aina hii ndio unaona hata wabunge wanalalamikia utekwaji nyara sio kwa sababu wanatupenda sana Bali kwa kuwa nao yanawakuta yaleyale yanayowakuta kina Roma na Kibanda.
Kuna haja ya kuwa imara zaidi na kuwa na umoja zaidi ili kuhakikisha kikundi kinachofanya haya kinabainika na kucjukuliwa hatua stahiki. Vinginevyo tutabaki tukilalama bila majibu ya msingi na muafaka kupatikana.
Juzi ilikua Ben Saanane ,ikaja Bashe, Mara Roma na wenzake hujui itakuja kwa nani?
Je serikali imeshindwa kutekeleza jukumu hili la kulinda raia na mali zao au ndio nimeshindwa hata kutoa majibu?
Au ndio inawajua wahusika Wa matukio haya?
Nawasilisha...