Usalama wa watembea kwa miguu barabarani

Usalama wa watembea kwa miguu barabarani

THE MAYA EMPIRE

Senior Member
Joined
May 6, 2018
Posts
106
Reaction score
149
Iko hivi,mabishano makubwa sana yameibuka ndani ya wanajamii juu ya upande upi wa barabara ambao mtembea kwa miguu yampasa apite ili asiweze kupata ajali ya kugongwa na magari yajayo nyuma yake au mbele yake au yale yanayo overtake gari jingine kila upande sehemu ambako hakuna njia rasmi za watembea kwa miguu

MOJA:::BAADHI WANASEMA GARI UNAYO ONGOZANA NAYO IKUPITE AU UIONE UPANDE WAKO WA KULIA

MBILI:::WENGINE WANASEMA GARI UNAYO ONGOZANA NAYO IKUPITE KUSHOTO KWA HIYO WEWE UPISHANE AU UIANGALIE KWA MBELE GARI INAYOKUJA MBELE YAKO NA SIYO UTEMBEE UPANDE WA GARI UNAYOKUJA NYUMA YAKO NA IKUPITE

Huu mjadala pia ukawapa ukakasi hata watalaamu wa masuala ya usalama barabarani hususani askari polisi ambao ni trafiki

Wajuvi wa mambo,njooni tuelimishane huku
 
kama vile magari yapitavyo ndio watembea kwa miguu yawapasa iwe hvo hvo
Kama nimekuelewa ukisema kwamba gari unayo ongozana nayo tembea pembeni yake au ikupite upande huo huo kwa maana nyingine gari unayo ongozana nayo ikupite mkono wako wa kulia
 
Siku zote mwenda kwa miguu kulingana na sheria zetu hapa Tz anatakiwa apite kulia mwa barabara na gari ipite kushoto mwa barabara.Ila watu wengi hawalijui hili la waenda kwa miguu hivyo hujikuta wakipita upande ule ule wa kushoto ambako magari hupita.
 
Siku zote mwenda kwa miguu kulingana na sheria zetu hapa Tz anatakiwa apite kulia mwa barabara na gari ipite kushoto mwa barabara.Ila watu wengi hawalijui hili la waenda kwa miguu hivyo hujikuta wakipita upande ule ule wa kushoto ambako magari hupita.
Mmhh hiyo ni sheria na unajua kwenye maarifa ya jamii tuliambiwaje?

Mtembea kwa Miguu apite upande wa kushoto wa barabara.

Nakumbuka vyema hiko kipande kwakua mara nyingi tulikua tunacheka juu ya aliyeamua mtembea kwa miguu kupita kushoto.
 
sijui sheria inasemaje kuhusu hili ila kwangu mimi huwa naona salama tena bila kuwa na hofu kutumbea upande tofauti na magari kwani naona gari inayokuja upande wangu kwa urahisi bila kugeuka geuka nyuma, siunajua tena mtu ana side mirror..
 
Huu mjadala ni mzito cha muhim ni kuwa tu makini unapokuwa barabarani
 
Hivi sheria inasemaje kule karikoo mtaa wa msimbazi watu wanapita kwenye barabara ya magari na sehemu za waenda kwa miguu kupewa machinga wapange bidhaa zao ?hali kadhalika kule gerezani,ubungo mataa ?
Nataka nijue aliyewaruhusu alitumia sheria gani???
 
Back
Top Bottom