Usalama wa taifa hawana meno

Status
Not open for further replies.

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,276
6,623
Nimetafakari kwa muda mrefu, ni miongoni mwa watu ambao kwa kiasi
Kikubwa nimekuwa nikiilaumu idara hii nyeti kuwa haifanyi kazi yake
Ipasavyo, nimegundua kuwa siko sahihi.

Ninachokiona hapa ni kuwa idara ya usalama wa Taifa imeng’olewa meno
na wanasiasa hivyo kuwa fanya wanasiasa ndio wapange idara iwe vipi na
iendeshwe vipi badala ya usalama wa Taifa kupanga siasa iwe vipi na iendeshwe
Vipi. Nahisi hawa jamaa wamekuwa wanafanya kazi ya ziada ya kuishauri serikali
Lakini inakuwa ngumu kutokana na hicho nilichokieleza.

MAONI YANGU:
Mkurugenzi wa usalama wa Taifa awajibike moja kwa moja kwa wananchi na
Si kwa Rais, ninachokusudia hapa ni kuwa kama kuna tatizo lolote ambalo
Linatakiwa kutolewa ufafanuzi na usalama wa Taifa au hata kama Mkurugenzi
Wa usalama wa Taifa anataka kuwajibishwa basi jukumu hilo lisiwe la Rais
Na badala yake lifanywe na Bunge moja kwa moja. Kama ni kujitetea n.k Mkurugenzi
Ajitetee mbele ya bunge ambalo ndilo linawakilisha wananchi.

Hili litasaidia Watu hawa kufanya kazi kwa uhuru zaidi na kwa manufaa ya Taifa.
Tutamlaumu sana OC lakini hana meno na anawajibika kwa Bosi wake ambaye ni
Raisi. Inakuwa ngumu hata kufuatilia ishu za maswaiba wa Rais, lakini likishapewa
meno ni jambo rahisi.
AMANI KWENU.
 
Hebu twambie zaidi, umejuaje kwamba Usalama ya sasa haina meno? Ni kipi kimekushawishi kufikiri kwamba usalama wa taifa hausikilizwi na JK? Je unajua kwamba usalama wa taifa kuna mambo wanayagundua yanayohitaji kufanyiwa kazi haraka. Je wakiwajibika kwa bunge ambalo linakaa mara chache kwa mwaka utekelezaji utakuwaje?

Tafakari.

Tiba
 
Hebu twambie zaidi, umejuaje kwamba Usalama ya sasa haina meno? Ni kipi kimekushawishi kufikiri kwamba usalama wa taifa hausikilizwi na JK? Je unajua kwamba usalama wa taifa kuna mambo wanayagundua yanayohitaji kufanyiwa kazi haraka. Je wakiwajibika kwa bunge ambalo linakaa mara chache kwa mwaka utekelezaji utakuwaje?

Tafakari.

Tiba
Kwamba hausikilizwi ipasavyo hilo halina shaka na huenda hata wewe
unafahamu isipokuwa unataka kuchimba zaidi kutoka kwangu. Umenambia
nitafakari zaidi.......... Hebu nitoe mfano mmoja tu, iwapo kuna ishu nzito
inamuhusu mtoto, mke, mama, rafiki n.k wa muheshimiwa Raisi huoni ugumu
ambao idara unakabiliana nao hapo?

Kama Serikali inasikia kutoka kwa usalama wa Taifa basi Idara yetu imeoza
jambo ambalo sikubaliani nalo.

NINACHOKIAMINI.
WANASIASA WETU WANAPENDA KUSIKIA WANACHOTAKA KUKISIKIA NA
HAWAPENDI KUKISIKIA WANACHOTAKIWA KUKISIKIA.......... Tfakari.

 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom